Je,Mabadiliko ya mswada wa kodi Marekani utawanufaisha maskini au matajiri?

mswada

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Je,mabadiliko ya mswada wa kodi Marekani utawanufaisha maskini au matajiri?

Maseneta wa Marekani wanajadili mswada ambao unaweza kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa Kodi ambao umekuwepo kwa miongo mingi nchini Marekani.

Wabunge wa bunge la wawakilishi awali walipiga kura upande wa mabadiliko makubwa ambayo ikiwa yatapitishwa itakuwa ni mafanikio ya kwanza makubwa ya Rais Trump katika utawala wake.

Kura katika Seneti inategemewa katika saa chache zijazo. Hata hivyo, maamuzi ya mwisho yatalazimika kusubiri hapo baadae ambapo mswada utakuwa umerejeshwa Bungeni kwa sababu ya kukamilisha utaratibu ,kabla ya rais Trump kuweka saini ili ipitishe kuwa sheria.

Maelezo ya picha,

Wabunge wa bunge la wawakilishi awalipiga kura ya mabadiliko ya mswada wa kodi

Upande wa Republican wanasema mabadiliko haya yatawasaidia watu wa kipato cha kati kwa kuwa yataweza kuongeza ajira,kupunguza makali ya kodi ,kuwepo kwa malipo ya juu,kuongezeka kwa kasi ya maendeleo na uhuru wa kutoka eneo moja mpaka lingine pamoja na kua na uchumi imara ambao utawanufaisha kila mmoja katika hali yake.

Huku Democrats wanasema mabadiliko hayo yanawanufaisha makampuni makubwa na matajiri.