Bunge la Uganda lajadili ukomo wa Urais kwa siku ya tatu

Bunge la Uganda Haki miliki ya picha CHARLOTTE COSSET
Image caption Bunge la Uganda

Bunge la Uganda limeanza kikao chake cha tatu cha kujadili mswada utakaomruhusu Rais Yoweri Museveni kugombea kwa awamu ya sita.

Vurugu kati ya wabunge na vikosi vya usalama zilitokea siku ya Jumanne wakati muswada huo ulipoanza kujadiliwa.

Mwandishi wa BBC Catherine Byrahunga anasema taifa hilo linasubiri kuona namna ambavyo wabunge hao watapiga kura katika swala hilo nyeti la kubadilisha katiba.

Image caption Wabunge wa Uganda wakipigana baada ya kuhitilafiana

Mipango ya kutoa ukomo wa umri wa Rais imepelekea kuwa na maandamano nchini Uganda.

Wengi wanaona kama mpenyo wa Yoweri Museveni kuwa Rais wa maisha.

Wakati huo huo , wafuasi wake wanasema kuwa wanaweza kupigia kura ya kumtoa wakati wowote.

Lakini wapinzani wanahisi kuwa uchaguzi nchini Uganda haujawahi kuwa huru na hautakuwa huru kwa siku za usoni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii