Wahubiri na watoto 100 wakamatwa na polisi katika madrassa Kenya

Wahubiri na watoto 100 wakamatwa na polisi katika madrassa Kenya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahubiri na watoto 100 wakamatwa na polisi katika madrassa Kenya

Zaidi ya wanafunzi thelathini nchini Kenya pamoja na waalimu wanne wanahojiwa na polisi baada ya kukamatwa katika shule moja ya kiislamu karibu na mji wa Mombasa pwani ya Kenya.

Karibu watoto mia moja walizuiliwa baada ya maafisa wa usalama kuvamia madrasa moja siku ya jumanne lakini wengi wameachiliwa. Vyombo vya habari nchini Kenya vimesema operesheni hiyo ya kuwakamata wanafunzi inahusiana na vita dhidi ya ugaidi na ilishirikisha mashirika ya polisi wa kigeni.

Haijulikani ni kwa nini uvamizi huo ulifanyika katika mji wa Likoni pwani mwa Kenya.

Hatahivyo ripoti kadhaa zinasema kuwa vikosi vya usalama vya kimataifa vya Marekani na Uingereza vilidaiwa kuhusika

Vyombo vya habari vinahusisha uvamizi huo na eneo moja la kukuza ugaidi mbali na biashara haramu ya kusafirisha watoto inayohusisha mataifa kadhaa na mabara.

Gazeti la The Star liliripoti kwamba watoto hao ni wa hadi umri wa miaka mitano na wanatoka umbali wa Marekani, Uingereza na Canada pamoja na mataifa mengine ya bara Afrika.

Duru ya polisi ambayo imekataa kutajwa iliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba shule hiyo ya madrassa ilikuwa kituo cha kuwapatia wanafunzi mafundisho ya kuwa na itikadi za wapiganaji na kimekuwa kikichunguzwa kwa mara kadhaa.

Sheikh Hassan Omar, ambaye ni afisa mkuu katika baraza la maimamu na wahubiri nchini Kenya CIPK , amboa ni mwavuli wa viongozi wa kidini nchini Kenya aliambia waandishi kwamba watoto hao walikuwa wakilala wakati kundi la maafisa wa polisi wa kigeni pamoja na wale wa nchini walipovamia.

Huwezi kusikiliza tena
Wakristo na Waislamu waonyesha umoja Kibera Kenya
Huwezi kusikiliza tena
Huenda juhudi za Kenya zinachangia ugaidi

Kuna takriban wanafunzi 100 na walimu wanne wa madrassa ambao wamekamatwa na kuzuiliwa katika makao makuu ya polisi na hakuna mtu anayesema ni uhalifu gani waliotenda.

Afisa mwandamizi wa polisi aliambia Reuters kwamba watoto hao wataachiliwa huru mmoja baada ya mmoja baada ya kuhojiwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii