Watu 2 wafariki katika moto uliochoma klabu ya burudani Kenya

Polisi nchini Kenya wanasema watu wawili wameuawa baada ya moto kuzuka kwenye klabu ya burudani nje ya mji wa Kisumu . Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Polisi nchini Kenya wanasema watu wawili wameuawa baada ya moto kuzuka kwenye klabu ya burudani nje ya mji wa Kisumu .

Polisi nchini Kenya wanasema watu wawili wamefariki baada ya moto kuzuka kwenye klabu ya burudani nje ya mji wa Kisumu .

Wameieleza BBC kuwa idadi ya watu huwenda ikaongezeka kwa sababu baadhi ya watu wamenaswa ndani ya jengo hilo.

Wazima moto bado wamefanikiwa kuuzima moto huo ulioanza kutoka ghorofa ya kwanza.

Polisi wanadhani kuwa hitalafu ya umeme ndio chanzo cha moto huo katika klabu ya Dream City ambayo pia ina vyumba vya wageni.

Watoa huduma ya kwanza, wametoa miili miwili ilioungua kutoka vyumba vilivyochomeka kwa mujibu wa kamanda wa polisi John Kamau.

Kamanda Kamau ameongezea kuwa watu wane wamenusuruka na kutolewa kutoka jengo hilo.

Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa wengine walijiokoa kwa kuruka nje kupitia madirisha