Wabunge wapitisha muswada wa ukomo wa rais Uganda kusomwa kwa mara ya pili

Bunge la Uganda limepitisha muswada wa ukomo wa rais kwa raujndi ya kwanza Haki miliki ya picha Twitter/bunge la Uganda
Image caption Bunge la Uganda limepitisha muswada wa ukomo wa rais kwa raundi ya kwanza

Muswada tata wenye lengo la kuondoa ukomo wa umri kwa mgombea urais nchini Uganda umeshinda hatua ya kwanza kwa kura nyingi.

Zaidi ya thuluthi mbili ya wabunge walipitisha mswaaada huo na kutoa nafasi kwa bunge kuanza kuulijadili mswaada huo, ibara moja baada ya nyengine na hatimaye kuupigia kura na kuwa sheria.

Chama tawala cha Uganda National Resistance Movement NRM kinapania mswaada huo upitishwe leo Jumatano kabla ya bunge kwenda likizo ya Krismasi.

Sasa muswada huo utajadiliwa kipengele baada ya kipengele na kupita kwenye kura ya mwisho .

Chama tawala kinataka muswada huo upitishwe mwisho wa siku ya leo, Jumatano.

Spika wa bunge la Uganda, Rebecca Kadaga siku ya Jumanne alilazimika kusimamisha mjadala wa muswada huo baada ya mbunge wa upinzani Lucy Akello kulalamika kuwa kulikuwa na wanajeshi kwenye moja ya kumbi za bunge inayotumika kufanya ibada.

Mwandishi wa BBC Patience Atuhaire, alielezea kuwa baadhi ya wabunge waliorudi kutoka kuchunguza ukumbi huo walisema kuwa walipata chupa zenye mikojo, ambazo wanajeshi hao walikuwa wanatumia kujisaidia.

Walisema pia wamepata vyombo vilivyotumika na mabaki ya chakula.

Baadhi ya wabunge walijaribu kuvipeleka vyombo hivyo bungeni kabla ya kipindi kuanza lakini maafisa wa usalama walivinyakua.

Huwezi kusikiliza tena
Wabunge wapigana makonde Uganda

Mwandishi wa BBC Patience Atuhaire anasema, hali ilikuwa ya taharuki ndani ya ukumbi wa bunge na mhemko ni mkubwa wakati wabunge wanaposema maeneo yao ya ibada yamedharauliwa

Kumbi zote za ibada za Wakatoliki na Waprotestanti zinaelezwa kutumika na wanajeshi.

Kisa hicho kiliwashutua raia wangi wa Uganda.

Maafisa wa polisi na wale wa kijeshi walipelekwa nje ya bunge pamoja na maeneo mengine ya mji .

Mamlaka inasema kuwa wamejiandaa dhidi ya ghasia wakati wa mjadala.

Bunge linatarajiwa kuendelea siku ya Jumanne mchana.Wakati wa makabiliano kati ya wabunge wa upinzani mnamo mwezi Septemba , wanajeshi kutoka katika kikosi maalum waliokuwa wamevalia sare za raia waliingia katika bungeni na kuanza kuwapiga na kuwakamata wabunge.