Swansea City yamtimua kocha Paul Clement

Paul Clement Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement

Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo msimu huu.

Clement mwenye miaka 45 alichukua jukumu la kuiongoza Swansea, mwezi Januari mwaka huu na kuisaidia kutoshuka daraja na kumaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita.

Katika msimu huu mpaka sasa Swansea wamecheza michezo 18, na wameshinda michezo mitatu ya ligi wakiwa wanaburuza mkia kwa alama 12.

Mwenyekiti wa Swansea Huw Jenkins, ametoa taaarifa kwa kusema klabu imelazimika kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia timu kufanya vizuri.