Ramaphosa aahidi kuimarisha uchumi wa Afrika Kusini

Cyril Ramaphosa amekuwa kiongozi mkuu wa ANC baada ya kuwashinda wapinzani wake akiwemo Nkosazana Dlamini Zuma
Image caption Cyril Ramaphosa amekuwa kiongozi mkuu wa ANC baada ya kuwashinda wapinzani wake akiwemo Nkosazana Dlamini Zuma

Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake.

Image caption Ramaphosa na Zuma awali walikua marafiki wa karibu

Amesema kuwa kikao cha kamati kuu pia kimeahidi kurudisha ardhi muhimu ambazo zilikua mikononi mwa wasiohitajika ikiwa ni lengo la kukuza sekta ya kilimo.

Amemsifu mpinzani wake wa karibu aliyembwaga kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa ANC Nkosazana Dlamini Zuma kuwa ni jasiri na mchapa kazi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii