Catalonia kufanya uchaguzi wake mkuu leo

Serikali ya Madrid inasema hali sasa ni shwari
Image caption Serikali ya Madrid inasema hali sasa ni shwari

Raia wa Catalonia leo hii watachagua viongozi wao wapya, katika uchaguzi ambao serikali kuu ya Uhispania inaamini utamaliza msuguano wa kisiasa unaoendelea.

Serikali kuu ya Madrid iliuvunja utawala uliokuwepo awali, baada ya kuandaa kura ya maoni iliyodaiwa kutofuata kanuni, iliyotaka uhuru wa eneo hilo.

Image caption Watu wengi wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu

Rais wa Catalonia aliyeondolewa madarakani, Carles Puigdemont, amekuwa akiendeleza kampeni zake za kujitenga na Madrid akiwa uhamishoni nchini Ubelgiji kwa kupitia mitandao ya kijamii.

Image caption Mwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania

Takwimu zinaonyesha kuwa vyama vinavyotaka kujitenga na vile vinavyotaka kusalia kwenye serikali ya Madrid vinalingana katika kura za maoni.

Mwandishi wa BBC wa eneo hilo anasema kuna kila dalili kwa uchaguzi huukuibua tena hisia za kutaka kujitenga kuliko kutatua matatizo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii