Gari lajeruhi umati wa watu Melbourne, Australia

Polisi wakiokoa majeruhi wa ajali hiyo
Image caption Polisi wakiokoa majeruhi wa ajali hiyo

Gari moja lililokuwa kwenye mwendo wa kasi limewagonga na kuwajeruhi watu kadhaa katika mji wa Melbourne nchini Australia.

Picha kutoka kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakiwa wameanguka chini, wakitokwa na damu karibu na gari hilo jeupe.

Baadhi ya waliojeruhiwa ni mtoto mdogo ambaye yupo katika hali mahututi.

Image caption Polisi inasema bado uchunguzi unaendelea juu ya mtuhumiwa wa tukio hilo

Polisi inasema inaamini kitendo hicho ni cha kukusudia na wanaendelea na uchunguzi.

Dereva wa gari hilo pamoja na mtu mwingine aliyekuwa nae wamekamatwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii