Uimbaji wa makundi husaidia kupunguza magonjwa ya akili

Kundi la muziki

Chanzo cha picha, SYHO

Maelezo ya picha,

Kundi la muziki

Uimbaji wa makundi unaweza kuwasaidia watu wanaougua ugonjwa wa akili, kwa kuwafanya kujihisi wenye thamani na kuongeza ujasiri wao, kulingana na utafiti.

Watafiti wa Chuo kikuu cha Uimbaji cha East Anglia wamesema mradi wa Sing Your Heart Out , umewasaidia watu ambao walikuwa wakiungua ugonjwa wa akili kupata nafuu.

Watafiti hao wameisihi jamii kubuni makundi wa uimbaji.

Penny Holder mwenye umri wa miaka 67, ambaye ameishi na ugongwa wa akili wa bipolar kwa maisha yake yote amesifu uimbaji wa makundi kwamba umeweza kubadilisha maisha yake kwa miaka 13 ambayo ameshiriki katika uimbaji.

Chanzo cha picha, SYHO

Maelezo ya picha,

Penny Holder,ameungua ugonjwa wa bipolar maishani mwake

Holder, amesema uimbaji huo wa pamoja umefanya maajabu katika maisha yake.

''Uimbaji ni kitu kizuri, ambao sijawahi kufanya maishani mwangu. Umeimarisha mazingara yangu ,na wenzangu kwani sisi husaidiana.''

''Mimi niliona ugumu kujihusisha na watu na hata kuwaamini siku za kwanza nilipoanza kujiunga na kundi hilo, lakini nilifahamu nilihitaji kufanya jambo lolote ili kuyarudisha maisha yangu kuwa ya kawaida.''

''Lakini sikutaka kukaa na kunywa chai na biskuti .''

Watafiti hao wameongeza kwamba uvutaji wa pumzi wakati wa kuimba umedhihirisha kuwa bora kwa mwili wa binadamu.