AU: Jeshi la Somalia halina uwezo wa kulinda taifa hilo

AU: Jeshi la Somalia halina uwezo wa kulinda taifa hilo Haki miliki ya picha AFP
Image caption AU: Jeshi la Somalia halina uwezo wa kulinda taifa hilo

Jeshi la Somalia haliko tayari kuanza operesheni za kiusalama nchini humo ,ijapokuwa baadhi ya vikosi vya Umoja wa Afrika vimeanza kuondoka nchini humo, kulingana na mkuu wa ujumbe wa AU nchini humo.

Wanajeshi wa Somalia hufanyia kazi kampuni za usalama za kibinafsi huku wale wanaosalia katika kambi wakiwa hawana silaha na vifaa vingine muhimu, Fransisca Madeira alisema katika taifa jirani la Kenya.

Muungano wa Ulaya, Uturuki , UAE na mataifa megine yana mipango ya kuwafunza wanajeshi wa Somalia.

Wanajeshi 1000 wa AU tayari wameondoka Somalia mwezi huu na wengine wengi wataondoka mwaka ujao.

Wamekuwa wakipambana na kundi la Kiislamu la al-Shabab, ambalo linahusishwa na al-Qaeda na linadhibiti eneo kubwa la taifa hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vikosi vya AU vimefanikiwa kukomboa baadhi ya maeneo yaliotekwa na wapiganaji wa al-Shabab

Ujumbe wa AU pia unakabiliwa na ufadhili mchache wa fedha na vifaa na kuna hofu kwamba kuondoka kwake kunaweza kurudisha nyuma ufanisi uliopatikana dhidi ya al-Shabab, ambao wamefurushwa katika miji mikuu katika kipindi cha miaka michache iliopita.

Mada zinazohusiana