Apple yakiri kupunguza kasi ya simu za iPhone

Mteja wa simu aina ya iPhone, Kampuni ya Apple imekiri kupunguza kasi ya simu hizo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mteja wa simu aina ya iPhone, Kampuni ya Apple imekiri kupunguza kasi ya simu hizo

Kampuni ya Apple imekiri wasiwasi uliokuwa na wamiliki wengi wa simu ya iPhone kwa kufichua kwamba imekuwa ikizipunguza kasi baadhi ya simu za zamani za Iphone.

Wateja wengi kwa muda mrefu wamekuwa na wasiwasi kwamba kampuni hiyo inapunguza kasi ya kupakia na kupakua ya simu za zamani wakati zinapoendelea kuzeeka kwa sababu betri ya simu hizo zinapungua nguvu kila wakati simu hizo zinapoendelea kuzeeka.

Apple imesema kuwa lengo lake lilikuwa kuimarisha maisha ya simu hizo kwa wateja wao.

Kitendo hicho kilithibitishwa baada ya mteja mmoja kusambaza utendakazi wake katika programu ya Reddit, akisema kuwa iPhone 6S imepunguza kasi kubwa kutokana na kuzeeka lakini ikaongeza kasi hiyo muda mfupi baada ya kuwekwa betri mpya.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Betri za lithium hupunguza nguvi zikiendelea kutumika

''Nilitumia simu aina ya Iphone 6 plus ya ndugu yangu na ilikuwa na kasi ya juu ikilinganishwa na yangu, ni wakati huo ndiposa nilibaini kuna tatizo'', aliandika Teckfire.

Mtandao wa kiteknolojia wa Geekbench baadaye ulizichanganua baadhi ya simu aina ya iPhones kupitia mifumo tofauti ya iOS na kubaini kwamba baadhi ya simu hizo zilikuwa zimepunguzwa kasi kwa makusudi,

Mada zinazohusiana