Guardiola bado ana hamu kumsajili Alexis Sanchez

Alexis Sanchez na mkufunzi wa ManCity Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexis Sanchez na mkufunzi wa ManCity Pep Guardiola

Manchester City bado ina hamu ya kumsajili Alexis Sanchez lakini huenda ikalazimika kusubiri hadi dirisha la uhamisho litakapofunguliwa ili kujaribu kupata saini ya mshambuliaji huyo wa Arsenal.

Jaribio la City kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 lilikubaliwa katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho mwezi Agosti lakini mpango huo ukashindwa kufua dafu.

Mkufunzi wa klabu hiyo Pep Guardiola tayari amefanya mazungumzo na usimamizi wa klabu hiyo kuhusu wachezaji anaolenga katika kipindi cha miezi 18.

Kuna hofu kwamba kumsajili Sanchez mnamo mwezi Januari kunaweza kuharibu mpangilio wa kikosi cha Guardiola .

Inaaminika kwamba City inadhani kwamba Arsenal inaamini kwamba kuendelea kumlazimisha mchezaji huyo kusalia katika klabu hiyo ni makosa na kwamba iko tayari kufanya biashara mwezi ujao.

Hatahivyo, huku kikosi cha Guardiola kikiwa na pointi 11 juu ya jedwali la ligi, kuna hisia kwamba ujio wa Sanchez unaweza kuvuruga kikosi hicho.

Mada zinazohusiana