Teknolojia 'inayowatambua' wapenzi wa jinsia moja

Haki miliki ya picha Stanford University
Image caption Teknolojia 'inayowatambua' wapenzi wa jinsia moja

Teknolojia 'inayowatambua' wapenzi wa jinsia moja

Utafiti ambao unafanyia majaribio teknolojia inayodaiwa kuwa na uwezo wa kutofautisha watu wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja umezua mzozo mkali kati ya waliotayarisha teknolojia hiyo na watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani wanadai kwamba wameunda programu ya kompyuta ambayo inaweza kuangalia uso wa mtu na maumbile yake na kutofautisha kati ya wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wengine.

Programu hiyo inaweza kutambua mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyabaini, wanasema.

Lakini watetezi wa haki za mashoga wameshutumu utafiti huo na kusema ni "hatari" na "sayansi isiyo na manufaa".

Lakini wanasayansi wanaohusika wamesema wanaopinga programu hiyo hawajaielewa vyema.

Maelezo ya kina kuhusu mradi huo yatachapishwa katika jarida moja kuhusu sifa za watu na saikolojia ya kijamii.

Gari la mwendo wa kasi zaidi duniani laanza majaribio

Gari lililoundiwa nchini Uingereza linaloweza kukimbia kasi ya kilomita 1,610 kwa saa, linafanyiwa majaribio yake ya kwanza huko Cornwall.

Bloodhound SSC linafanya mikimbio ya mwendo wa chini ya hadi kilomita 320 kwa saa katika uwanja wa ndege wa Newquay.

Likiendeshwa na Andy Green, gari hilo linalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mwendo wa kasi zaidi ardhini.

Jaribio hilo litafanywa kwenye barabara maalum iliyojengwa eneo la Nothern Cape nchini Afrika Kusini.

"Tumeunda gari lisilo la kawaida kabisa, lenye uwezo mkubwa na kasi ya juu zaidi katika historia." Andy Green aliambia BBC.

L'Oreal kutumia 3D kuunda nywele

Kampuni moja nchini Ufaransa imesema kwamba teknolojia sawa na ile inayotumiwa kupiga chapa vitu vya uhalisia, 3D, huenda ikatumiwa kuunda nywele za binadamu na hivyo kufaa wenye upara.

Nywele hizo baadaye zitaweza kupandikizwa kwenye watu waliopoteza nywele.

Kampuni ya L'Oreal inashirikiana na kampuni ya kupiga chapa viumbe hai ya Poietis, ambayo imeunda teknolojia ya kupiga chapa kwa kutumia laser ambayo inaweza kuunda sehemu za seli za viumbe.

Vinyweleo vya nywele havijawahi kuundwa kwa njia hii awali lakini kampuni hizo mbili zinatarajia kwamba zitaweza kustawisha teknolojia na kuwezesha kuundwa kwa vinyweleo hivyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Hata hivyo, shirika moja linaloangazia watu wanaopoteza nywele limesema bado ni mapema mno kwa watu kuanza kushangilia.

L'Oreal tayari hutumia ngozi iliyoundwa kwa teknolojia ya 3D kufanyia utafiti bidhaa za kutumiwa kwenye ngozi.

Nissan yazindua kiti cha gari chenye uwezo wa kutambua jasho

Nissan imeuzindua kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la binadamu ambacho kampuni hiyo inasema kuwa kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Teknolojia hiyo inayojulikana kama Soak, hubadlisha rangi ikiwa itatambua kuwa dereva atakuwa ameishiwa maji mwilini.

Utafiti wa walia uliofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University uligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa mengi sawa na madereva walevi.

Ngozi hiyo ya kiti iliyoundwa na kampuni moja nchini Uholanzi pia itawekwa kwenye usukani wa gari na viti vya mbele vya gari .

"Hii ni sehemu ya mpango mzima ambao sio tu wa kufuatilia tu gari bali pia dereva." alisema Prof Peter Wells.

Fifa yatetea teknolojia ya kutumia picha za video

Shirikisho la soka duniani Fifa limetetea mfumo mpya wa teknolojia ya Video uliobuniwa kuwasaidia Marefa kutoa maamuzi sahihi (VAR) kuwa teknolojia hiyo itafaa sana katika mchezo wa mpira wa miguu siku za mbeleni

Lengo shirikisho hilo la soka ni kuona teknolojia hiyo inatumika katika fainali za michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 ambazo pia zitachezwa Nchini Russia.

Rais wa Fifa Gianni Infantino amesema : "Tumeona namna teknolojia hii ya video inavyoweza kuwasaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi uwanjani.

Katika maelezo ya Fifa katika matukio matano yaliyotokea kwenye michuano ya kombe la mabara yakaamuliwa na teknolojia hiyo imeonyesha manne ni ya kuzidi na moja ni la mchezaji kushika mpira.

Kampuni kutumia ndege kuwafukuza wafanyakazi afisini Japan

Kampuni moja nchini Japan inapanga kutumia ndege zisizo na rubani kuwafukuza wafanyakazi wanaokosa kwenda nyumbani na kutaka kuendelea na kazi muda wao wa zamu ukimalziika.

Ndege hiyo zitakuwa zikipaa hadi walipoketi wafanyakazi wa kampuni ya Taisei na kuwachezea muziki.

Ndege hiyo maalum zitakuwa zinacheza wimbo maarufu wa Auld Lang Syne ambao mara nyingi hutumiwa kutangaza kwamba maduka au afisi zinafungwa.

Japan imekuwa ikikabiliana na tatizo lililokithiri la wafanyakazi kufanya kazi muda wa ziada kupita kiasi, tatizo ambalo limekuwa likiathiri afya ya wafanyakazi na wakati mwingine hata kusababisha vifo.

Teknolojia kuwasaidia wakulima wa miwa

Idadi kubwa ya wakazi wa wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro wanajulikana kwa ukulima hasa wa zao la mpunga na muwa kwa ajili ya kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wakulima hawa walianza kukata tamaa ya ukulima huku wengine wakijaribu kufanya shughuli mbadala kama vile kujiingiza katika biashara ndogo ndogo. Hii ni baada ya mbegu za miwa walizokuwa wakitumia kupoteza ubora wake, na matokeo yake kushindwa kustahamili mabadiliko ya tabia nchi na hatimae kuvamiwa na magonjwa. Masoud Mohamed Mshame ambae ni mkulima wa miwa kutoka wilayani humo anakiri kwamba kila mwaka, mavuno yalikuwa yakipungua.

"Kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa, mwaka jana na mwaka juzi, tulivuna mapato ya chini tofauti na kipato tulichokuwa tunategemea siku za nyuma. Kwa miaka mitatu iliyopita, tulikuwa tunavuna kuanzia tani 30. Ilipofika mwaka jana, tulivuna hadi tani 20 na chini ya hapo," amesema Masoud.

Hivi sasa hali imeanza kubadilika. Baadhi ya wakulima wanaonekana kujawa na hamasa na matumaini ya kufanya vizuri katika kilimo. Hii ni baada ya kufikiwa na mradi wa endelevu maarufu kama SUSTAIN ambao umejikita zaidi katika kuzalisha mbegu za miwa ambazo baada ya kufanyiwa utafiti na Kituo cha Utafiti wa Miwa Kibaha, imethibitika kwamba zina ubora na uwezo wa kustahamili ukame.

Blackberry yaishtaki Nokia kwa wizi wa teknolojia

Kampuni ya simu ya Blackberry inaishtaki Nokia kuhusu madai kwamba kampuni hiyo ya Finland imetumia uvumbuzi wake bila ruhusa.

Madai hayo ya ukiukaji yanahusisha teknolojia inayotumika katika 4G pamoja na mitandao mingine ya simu.

Kampuni hiyo ya Canada inadai kwamba transmita za Nokia pamoja na programu nyengime zinatumia teknolojia yake.

Nokia imeambia BBC kwamba inaliangazia swala hilo.

''Tunajua kwamba kuna malalamishi ,tutayajadili madai yaliotolewa na kuchukua hatua zinazohitajika kutetea haki zetu'',alisema msemaji.

Wasichana waliobobea katika teknolojia Kenya

Je, unataka programu ya kulipia nauli kwenye gari, ama, programu ya kutafuta viungo vya mwili kwenye simu yako? Wasichana nchini Kenya wanatengeneza programu hizo, chini ya uongozi wa shirika la kimataifa linalowapa wasichana elimu ya kutengeneza programu za simu.

Harriet Karanja, 16, alikuwa kwenye foleni akisubiri kununua tiketi ya kusafiri kwa basi jijini Nairobi, wakati mama mmoja aliyekuwa kwenye foleni alipokonywa mali yake na wezi.

Aliposimulia tukio hilo kwa wenzake wanne shuleni, aligundua kwamba pia wao walikuwa wameshuhudia tatizo sawa na hilo.

"Itakuwaje iwapo tutabuni njia ya kuwaondoa watu kwenye foleni kununua tiketi?" Harriet akauliza.

Baadaye waliamua kutengeneza programu ya simu (App) ya kurahisisha ununuzi wa tiketi za usafiri, kwa magari ya masafa marefu.

"Programu hii inakuongoza hadi kwenye kituo cha basi kwa kutumia teknolojia ya kugundua maeneo (GPS). Badala ya kwenda kupanga foleni, utaenda tu kuabiri."

Wameipa jina 'M- Safiri'

Wanawake na teknolojia nchini Kenya

Kenya ni mojawapo wa mataifa barani Africa, ambapo asilimia kubwa ya raia wanapokea huduma za mitandao.

Hata hivyo, kulingana na utafiti wa wakfu wa World Wide Web, ni 20% pekee ya wanawake katika vitongoji duni katika mji mkuu wa Nairobi wanaopata huduma za mitandao.

Utafiti huo aidha umebaini kwamba 57% ya wanaume wanapokea huduma hizo.

Na huku ulimwengu ukiadhimisha wiki ya mitandao ya kijamii na teknolojia, mashirika mbalimbali yamejitokeza kupunguza pengo la kijinsia katika matumizi ya mitandao nchini Kenya.

Njia mbalimbali za ubunifu zinatumika kuwafunza wanawake.

Rais wa China ataka jeshi lake kukumbatia teknolojia mpya

Rais Xi Jinping wa China ameambia mkutano mkuu wa maafisa wa vyeo vya juu kwenye jeshi kuwa lazima idara hiyo ifanya mabadiliko ili iweze kuendesha shughuli zake kwa mtindo wa mamboleo.

Bwana Xi alisema kwa sasa jeshi linapaswa kuwa na watu wachache na silaha za kisasa kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya kitekinolojia.

Alisema kuwa kwa wakati huu silaha za kisasa zilizo na teknolojia mamboleo ndizo zinazohitajika katika ushindi wowote wa kivita.

Chanjo ya watoto huenda ikatolewa mara moja

Teknolojia ambayo huenda ikapelekea chanjo ya watoto kutolewa mara moja kwa kila mtoto imebuniwa na watafiti nchini Marekani.

Chanjo hiyo itakayotolewa mara moja kwa mpigo itashirikisha dawa zote katika sindano moja ambazo zitakuwa zikifanya kazi kwa muda utakaohitajika ili kumkinga mtoto na magonjwa yanayolengwa.

Teknolojia hiyo imeonakana kufanya kazi miongoni mwa panya katika jarida la sayansi.

Watafiti wanasema teknolojia hiyo inaweza kuwasaidia wagonjwa duniani.

Chanjo ya watoto husababiha vilio na machozi na nyingi hupewa watoto kwa muda tofauti.

Kundi moja la watafiti katika chuo cha kiteknolojia cha Massachusetts kimebuni chanjo ambayo inashirikisha dawa zote za chanjo anayopewa mtoto.

Matukio 10 makuu mwongo mmoja wa iPhone

Kampuni ya Apple inaadhimisha miaka 10 tangu kuzinduliwa kwa simu zake za kisasa aina ya iPhone na inatarajiwa kwamba watazindua simu nyingine itakayokuwa na mabadiliko makubwa tangu kuzinduliwa kwa simu hizo.

Miongoni mwa mengine, muundo wa simu zenyewe unatarajiwa kubadilika, zitakuwa na uwezo wa kumtambua mtu kwa kuchunguza uso wake na pia kutakuwa na mabadiliko mengine kuongeza mtazamo wa uhalisia kwenye simu zenyewe.

Wachanganuzi kadha wamedokeza kwamba huenda bei ya simu hizo ikapanda zaidi.

Katika ulimwengu ambao simu za smartphone zimekuwa kama sehemu ya binadamu, ni rahisi kusahau jinsi simu za iPhone zilipozinduliwa na Steve Jobs mwongo mmoja zilivyowashangaza wengi na jinsi mjadala mkali ulivyozuka kuhusu iwapo zingebadilisha teknolojia mbalimbali za simu.

Kuadhimisha miaka 10 ya iPhone, tumechagua matukio makuu 10 katika kipindi hicho ambayo yalibadilisha sana mambo.

Taarifa za siri za kampuni ya Apple zafuja

Taarifa kuhusu simu mpya za iPhone na vifaa vingine vya Apple ambavyo havijazinduliwa zimefuja.

Mitandao miwili iliruhusiwa kuona aina mbili ya tekenolojia ya iOS kabla ya siku kuzinduliwa.

Taarifa zilizofichuliwa ni za simu ya iPhone X pamoja na ya simu mbili aina ya iPhone 8.

Mwandishi mmoja wa masuala ya teknolojia huo ndio ufujaji mkubwa zaidi katika kampuniya Apple.

Baadhi ya Apps za iPhones na ipads za Apple zitasimama

Wamiliki wa simu za iPhones na iPads waliotengeneza toleo la hivi karibuni la mfumo wa simu ya mkononi ya Apple watabaini kuwa baadhi ya apps za zamani zitasita kufanya kazi.

Hatua hiyo itaathiri kwa ujumla apps ambazo zimekuwa hazijafanyiwa marekebisho mapya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Ingawa nyingi zitaacha kutumiwa na wabunifu wake, wamiliki wake bado wataendelea kutumia baadhi yake mara kwa mara.

Haya ni matokeo ya kudhibitiwa kwa iOS 11 kuendesha apps zilizoandikwa katika kile kinachofahamika kama 64-bit code.

Namba hii inaonyesha ni kwa kiwango gani cha data kinachoweza kutengezwna ambacho kinaweza kutunzwa na simu - kadri namba inavyokuwa kubwa zaidi ndivyo kompyuta inavyokuwa na uwezo wa kufanya kazi.

Nissan yaunda magari mapya yanayotumia umeme

Kampuni ya magari ya Nissan imezindua magari mapya ya umeme, wakati inakabiliana na ushindani unaozidi kukua wa magari ya umeme

Aina hiyo mpya ya magari yanaweza kusafiri mwendo wa asilimia 50 zaidi baada ya kupata chaji, kwa mujibu wa kampuni hiyo.

Hata hivyo bado magari hayo hayajafikia mwendo wa magari wa Tesla na GM.

Magari hayo yanayofahamika kama 'Leaf' yanakabiliwa na ushindani mkali wakati sekta ya magari yanayotumia umeme inazidi kukua.

Huwezi kusikiliza tena
Wanawake wajifunza kutumia teknolojia Kenya

Mada zinazohusiana