Ulimwengu waonyesha umoja na mtoto wa Syria aliyejeruhiwa jicho

Picha za watu mitandaoni Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Picha za watu mitandaoni

Picha ya mtoto raia wa Syria ambaye alipoteza macho na kujeruhiwa mara kadhaa kichwani katika shambulio lililo ripotiwa kutekelezwa na serikali limezua gumzo na kuzua kampeini ya ushirikiano kwenye mtandao wa kijamii.

Karim, ambaye ana umri wa miezi miwili tu, alijeruhiwa pale mzinga ulipopiga na kulipua soko moja lililoko katika eneo linalomilikiwa na waasi mashariki mwa Ghouta, viungani mwa mji mkuu Damascus mnamo Oktoba 29. Mamake aliuwawa katika mkasa huo.

Eneo hilo lina takriban watu laki nne,mji na vijiji mashariki mwa Ghouta umezingirwa na wanajeshi wa serikali tangu mwaka 2013.

Licha ya kuwa eneo hilo kutengwa vita vmeongezeka katika wiki za hivi majuzi.

Zaidi ya watu 500 wanasubiri kuhamishwa ili kuokoa huduma za matibabu , pia kuna ukosefu wa chakula , mafuta ya taa na dawa na baridi inayokumba eneo hilo inatarajiwa kuongeza hali ngumu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption The Eastern Ghouta has been devastated by years of fighting

Babake Karim akizungumza na shirika la habari la Uturuki la Anadolu amesema mtoto wake anahitaji upelelezi wa mara kwa mara.

#SolidarityWithKarim imetumika Zaidi ya mara 26,000 tangu Jumatatu.

Picha za Karim zimesambazwa mara mia moja katika mitandao ya kijamii tofauti.

Watumizi wa mitandao hiyo wa Syria,wamechapisha picha wakifinika jicho lao la kushoto kudhihirisha uchungu ambao Karim anapitia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Habari ya Karim, imewagusa wanasiasa, wanahabari na wanaharakati kutoka Syria.

Habari ya Karim, imewagusa wanasiasa, wanahabari na wanaharakati kutoka Syria.

Wafanyikazi wa gazeti la Ujerumani Bild walipiga picha ya pamoja ''kudhihirisha hisia yao''kuhusiana na vita vinavyoendelea nchini Syria.

Kampeini hiyo iliifikia katika makao makuu ya umoja wa mataifa mjini New York siku ya Jumamosi,mwakilishi wa Uingereza Mattew Rycroft alimtaja mtoto Karim kwenye mkutano wa kamati ya usalama.

Mada zinazohusiana