Sudan kusini kusitisha mapigano kuanzia krismasi

one
Image caption Rais wa Sudan kusin,Salva Kiir

Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi wameweka saini ya kusitisha mapigano kuanzia siku ya krismasi,

hatua itakayomaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka mine. Makubaliano yalitiwa saini katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa katika mkutanoulioitishwa na IGAD.

Makuabliano yanaruhusu makundi ya makundi ya kutoa misaada kuwafikia wananchi waliobanwa katika maeneo ya mapigano.

Mara kadhaa makubaliano ya kusitisha vita yametiwa saini Sudan kusini lakini yote hayakutekelezwa.

Maelfu wamepoteza maisha na mamilioni kuyakimbia makazi yao kutokana na machafuko nchini Sudani kusini taifa ambalo lilipata uhuru miaka sita iliyopita.

Mada zinazohusiana