Ajax yatimua benchi lote la ufundi

sports Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dennis Bergkamp (upande wa kulia)

klabu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi imetimua benchi lake lote la ufundi kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo katikia michezo ya ligi ya Uholanzi na ulaya .

Waliotimuliwa ni kocha mkuu Marcel Keizer na msaidizi wake Dennis Bergkamp na pamopja na kocha wa Hennie Spijkerman.

Meneja mkuu Edwin Van De Sar na mkurugenzi wa kiufundi Marc Overmars pia wameondoka katika sehemu ya uongozi kwa sababu ya matokeo mabaya

Mlinzi wa zamani wa kimataifa wa uholanzi Michael Reiziger, na Winston Bogarde wamepewa mikoba ya kuingoza Ajax kwa muda.

Huku makocha wakubwa kwenye soka la Uholanzi kama Ronald Koeman na Frank De Boer wakitajwa kuwaq katika mpango wa muda mrefu.

Mada zinazohusiana