Uingereza kuanza kutumia hati mpya ya kusafiria 2019

Uingereza inasema mpango huu ni kuipa nchi hiyo nguvu zaidi
Image caption Uingereza inasema mpango huu ni kuipa nchi hiyo nguvu zaidi

Serikali ya Uingereza itaanza kutumia hati mpya za kusafiria mwaka 2019 baada ya kuondoka ndani ya umoja wa Ulaya.

Imesema kuwa itarudia mfumo wake wa zamani ambapo hati hiyo itakua na rangi za blue yenye nyeusi na dhahabu iliyokuwa ikitumika na wananchi wa Uingereza kabla ya kujiunga na umoja huo mwaka 1988.

Mawaziri wanasema hati hiyo mpya ya kusafiria itaonyesha uimara wa Uingereza, na wale waliounga mkono kujitenga na umoja wa Ulaya.

Serikali inasema mabadiliko hayo hayatagharimu chochote kwa wananchi wake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii