Mwanajeshi wa zamani aliyepanga shambulio la krismasi San Francisco akamatwa

Raia huyo wa Marekani hakujua kwamba alikuwa akizungumza na maafisa wa FBI Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia huyo wa Marekani hakujua kwamba alikuwa akizungumza na maafisa wa FBI

Maafisa wa ujesusi nchini Marekani wamemkamata mtu anayedaiwa kupanga njama ya kufanya mashambulio siku ya Krismasi katika mojawapo ya eneo maarufu la kuwavutia watalii katika mji wa San Francisco.

Everitt Aaron Jameson, mwenye umri wa miaka 39 ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi la majini la Marekani, ameshtakiwa kwa jaribio la kutoa usaidizi kwa shirika la kigeni linalohusishwa na visa vya ugaidi.

Bwana Jameson alifichua mpango wake kwa ajenti wa kisiri wa shirika la kijesusi la Marekani, FBI ambaye alimdhania kuwa ni mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la Islamic State.

Anadai kumwambia ajenti huyo kwama siku ya Krismasi ni siku nzuri sana ya kutekeleza shambulizi na kwamba hakuna haja ya kutafuta kufanya mpango wa kutoweka baada ya shambulio hilo kwa sababu yuko tayari kufa.

Mada zinazohusiana