Basi lililokuwa likiendeshwa na kijana wa miaka 16 lawaua watu 32 baada ya kuanguka mtoni India

Mabaki ya basi hilo yakitolewa katika mto baada ya kukosa mwewlekeo na kuanguka darajani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabaki ya basi hilo yakitolewa katika mto baada ya kukosa mwewlekeo na kuanguka darajani

Basi lililokua na abiria 50 nchini India limeanguka katika daraja moja na kuwaua takriban watu 32 lilipoingia katika maji Kaskazini mwa India kwa mujibu wa polisi.

Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na kijana wa miaka 16 lilipoteza mwelekeo kabla ya kuanguka mita 30 katika mto Banas.

Lilikuwa likiwabeba abiria kutoka eneo la Rajasthan kuelekea Ramdevji katika wilaya ya Sawai Madhopur kulingana na vyombo vya habari.

Polisi waliohojiwa na jarida la Hindustan wanasema kuwa dereva huyo ni miongoni mwa wale waliofariki likimtaja kuwa mtoto asiye na mafunzo ya udereva.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na kijana wa miaka 16 lilipoteza mwelekeo kabla ya kuanguka mita 30 katika mto Banas.

Wengi wa waathirika , ikiwemo wanawake na watoto walikufa maji kulingana na mamlaka.

Huduma za uokoaji zililazimika kukata mabaki ya basi hilo lili kuwaokoa manusura ambalo lilikuwa limezikwa chini ya daraja hilo.

Basi hilo baadaye lilivutwa nje ya mto huo.

Mada zinazohusiana