Watu wengi wahofiwa kufa kwenye mkasa wa moto Ufilipino

Burning shopping mall in Davao, the Philippines Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wengi wahofiwa kufa kwenye mkasa wa moto Ufilipino

Takriban watu 37 wanahofiwa kufariki katika mkasa wa moto, ambao uliteketeza maduka kadhaa katika mji ulio Kusini mwa Ufilipino wa Davao.

Kwa muda wa saa nne mfululizo, wazima moto walipambana na moto huo ili kuuzima.

Inaaminika moto huo ulianzia orofa ya tatu ya jumba hilo na kusambaa kwa kasi katika ghorofa za juu, na kuwafanya baadhi ya wafanyikazi kukwama humo.

Rais wa nchi hiyo Rodrigo Duterte alizuru maeneo ya janga hilo na kukutana na baadhi ya familia ambao wapendwa wao hawajulikani waliko.

Naibu meya wa mji huo, Paolo Duterte, ambaye ni mwanawe Rais Duterte, amesema matumaini ya kuwapata watu waliokwama humo wakiwa hai ni finyu mno.

Image caption Watu wengi wahofiwa kufa kwenye mkasa wa moto Ufilipino

Pia zaidi ya watu 200 wamethibitishwa kufa kwenye janga la mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi nchini Ufilipino baada ya Upepo mkali kugonga maeneo ya kusini mwa Kisiwa cha Mindanao.

Baraza kuu la kupambana na majanga ya asili nchini Ufilipino, linaongoza operesheni ya kujaribu kuwapa maelfu ya waathiriwa, maji safi ya kunywa na makaazi ya muda.

Huku msaada ukiwa bado haujawafikia waathiriwa katika maeneo ya ndani vijijini, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema kwamba Umoja wa mataifa uko tayari kutoa msaada wake.

Upepo huo mkali kwa jina Tembin, sasa unaondoka Ufilipino ukielekea Vietnam.