Uchaguzi Urusi: Mikutano yafanyika kumuunga mkono Alexei Navalny

Russian jailed opposition leader Alexei Navalny arrives for a hearing at a court in Moscow, 16 June 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mikutano yafanyika kumuunga mkono Alexei Navalny

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, ameuambia mkutano mmoja mjini Moscow kuwa uungwaji mkono mkubwa anaopata kwa sasa kote nchini Urusi, unathibitisha kuwa yeye ndiye anafaa kuwa Rais wa nchi hiyo badala ya Rais Vladimir Putin.

Bwana Navalny anapiga siasa kali ili jina lake lirejeshwe miongoni mwa orodha ya watakaowania kiti cha Urais nchini humo mwezi Machi mwakani.

Anahitaji majina 500 kwa kila miji 25 ambapo ana wafuasi wengi, na alipata kwa urahisi mno idadi hiyo katika mji mkuu Moscow.

Lakini mwezi Februari mwaka huu, tume ya uchaguzi mkuu nchini humo ilimzuia kwa miaka mitano kuwania kiti cha Urais kwa madai ya ubathirifu wa fedha.