Tunisia yapiga marufuku ndege za Emirates kutua mji mkuu Tunis

Emirates flight takes off Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Tunisia yapiga marufuku ndege za Emirates kutua mji mkuu Tunis

Tunisia imepiga marufuku ndege za shirika la Emirates kutua kwennye mji mkuu Tunis baada ya wanawake kadha raia wa Tunisia kuzuiwa kuabiri ndege za shirika hilo.

Hatua hiyo inakuja huku kukiwa na malalamiko makubwa nchini Tunisia kulaani hatua hiyo ya Emirates.

Wizara ya ulinzi ilisema kuwa marufuku hiyo itasalia hadi pale Emirates itakapoweka kuendesha shughuli zake kulingana na sheria na makubaliano ya kimataifa.

UAE ilisema kuwa tatizo la kuisalama lilisababisha hali hiyo.

Maafisa wa serikali ya Tunisia walisema kuwa UAE ilikuwa imepiga marufuku wanawake wa Tunisia kupitia nchi yake.

Siku ya Ijumaa serikali ya Tunisia ilisema kuwa ilikuwa imemuuliza balozi wa UAE kueleza kile kilikuwa kikiendelea na alikuwa ameambiwa kuwa hatua hizo zilikuwa ni za muda na tayari zilikuwa zimeondolewa.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa wanawake wa Tunisia walikuwa wamezuiwa kuabiri ndege za Emirate kwenda Dubai kwa siku kadhaa.

Tunisia imejaribu kuboresha uhusiano wake na UAE ulioharibika wakati wa mapinduzi mwaka 2011.

Mada zinazohusiana