Manowari ya Uingereza yaizuia ile ya Urusi huko North Sea

HMS St Albans (foreground) escorts the Russian vessel through the North Sea. Photo: 25 December 2017

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Manowari ya Uingereza yaizuia ile ya Urusi huko North Sea

Monowari ya jeshi la wa wanamaji wa Uingereza iliisindikiza ile ya Urusi katika bahari ya North Sea karibu na maji ya Uingereza siku ya Krismasi, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji wa Uingrreza.

Ilisema kuwa HMS St Albans ilisindikiza Admiral Gorshkov katika sehemu zilizo karibu na maji yake.

Urusi haijatamka lolote kuhusu kuhusu suala hilo.

Jeshi la Uingereza lilisema kuwa kumekwa na visa hivi karibuni ambapo vyombo vya majini vya Urusi vinapita karibu na maji ya Uingereza.

Mkuu wa jeshi la ulinzia nchini Uingereza Sir Stuart Peach, mapema mwezi huu alisema kuwa Uingereza na Nato wanahitaji kuweka kipaumbele suala la kulinda nyaya za mawasiliano ya mtandao zinazopiti baharini.

Alisema kuwa itakuwa piga kubwa na baya kwa uchumi ikiwa nyaya hizo zinatakatwa au kuharibiwa.

Nyanya hizo uunganisha sehemu tofauti za dunia kati ya nchi na mabara.

Katika taarifa jeshi la majini la Uingereza lilisema kwa HMS St Albans iliitwa tarehe 23 Disemba, kupiga doria na kuifuata manowari mpya ya Urusi ya Admiral Gorshkov ikipitia bahari karibu na maji ya Uingereza.

Lilisema kuwa meli hiyo ilisalia baharini siku ya Krismasi, ikichunguza chombo hicho cha Urusi.

"Sitakawia kulinda maji au kuvumilia uchokozi wowote," waziri wa ulinzi Gavin Williamson alisema.