Hasimu mkubwa wa Putin Alexei Navalny azuiwa kuwania urais

Russian opposition leader Alexei Navalny delivers a speech during a meeting with his supporters in Moscow

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Hasimu mkubwa wa Putin Alexei Navalny azuiwa kuwania urais

Kiongozi wa upinzni nchini Urusi Alexei Navalny amezuiwa kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Tume kuu ya uchaguzi nchi humo ilisema kwa kuwa Bwa Navalny hataweza kuwania kwa sababu alipatikana na makosa ya ufisadi ambayo anasema kuwa yamechochewa kisiasa.

Amewashauri wafuasi wake kususia uchaguzi huo wa mwezi Machi.

Bw. Navalny 41, ameonekana pakubwa kama mgombea pekee ambaye ana fursa ya kumkabili rais Vladimir Putin.

Akipata umaarufu kutokana na kampeni ya kupinga ufisadi na maanadamano dhidi ya Bw. Putin, Bw Navalny alihukumua kifungo cha nje cha miaka mitano mapema mwaka huu kwa mashtaka yanayohusu matumizi mabaya ya fedha.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Ella Pamfilova alisema kuwa tume yake inatekeleza sheria ambaya inamzuia Bw. Navalny.

Akijubu hatua hiyo iliyokuwa inatarajiwa, Bw. Navalny alisema kuwa kesi hiyo ilinuia kumzuia kuongea ukweli kuhusu hali ilivyo nchini Urusi na kuwa kumzuia kugombea kutawanyika mamilioni ya watu wa Urusi haki yao ya kupiga kura.

"Ni Putin pekee na mgombea ambaye alimchagua mwenyewe na ambaye sio tisho kwa njia yoyotew kwake ndio watashirikia, aliongeza.

Alisema atakata rufaa kwenye mahakama ya katiba ya Urusi.

Bw Navalny alisema Jumapili kuwa amekusanya sahihi 500 zilizohitajika kumwezesha yeye kugombea akiwa na matumaini kuwa hilo litaishinikiza tume ya uchaguzi kumruhusu kugombea.