Canada yamfukuza balozi wa Venezuela

Venezuelan President Nicolas Maduro speaks at the closing ceremony of the XVI Political Council of the Bolivarian Alliance for the People of Our Americas (ALBA) at the Convention Palace in Havana, on December 14, 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Nicholas Maduro

Canada imetangaza kuwa inamfukuza balozi wa Venezuela Wilmer Barrientos Fernández

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Chrystia Freeland alisema kuwa hatua hiyo ni jibu kwa kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wake wa cheo juu kutoka Venezuela mwishoni mwa wiki.

Venezuela iliilaumu Canada kwa kuingilia masuala yake ya ndani.

Cadana ilikuwa imeilaumu serikali ya Rais Nicholas Maduro kwa ukiuja wa haki za binadamu.

Zaidi ya watu 120 wameuawa wakati wa miezi kadha ya kuipinga serikali mapema mwaka huu.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Venezuela ilimlaumu bwana Kowalik (kushoto) kwa kupokea maagizo kutoka kwa Trump

Bi Freeland alisema kuwa Bw. Barrientos alikuwa tayari nje ya nchi na hataruhusiwa kurudi Cnada huku afisa mwingine wa kibalozi naye akitakiwa kuondoka.

Canada tayari ilikuwa imewawekea vikwazo maafisa wa vyeo vya juu wa Venezuela katika hatua ambayo iliikasirisha serikali ya Venezuela.

Venezuela pia ilimfukuza balozi wa Brazil Ruy Pereira, kutokana na madai kuwa serikali yake imekiuka sheria.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Zaidi ya watu 120 wameuawa wakati wa miezi kadha ya kuipinga serikali mapema mwaka huu.

Marekani ilimwekea vikwazo Maduro na utawala Trump umemtaja kuwa mtawala wa kiimla.

Upinzani umemlaumu Bw Maduro na mtangulizi wake hayati Hugo Chavez kwa kuharibu uchumi wa nchi kutokana na sheria zao za kisoshiolisti.