Taarifa kuhusu tafiti zilizofanyika 2017

Image caption Utafiti mpya unaashiria kwamba ni kweli wanaume hutatizwa na mafua zaidi ya wanawake, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa dhana kwamba huwa kuna mafua ya wanaume.

Utafiti: Wanaume hulemewa na mafua zaidi ya wanawake

Utafiti mpya unaashiria kwamba ni kweli wanaume hutatizwa na mafua zaidi ya wanawake, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa dhana kwamba huwa kuna mafua ya wanaume.

Watafiti nchini Canada wanasema wamepata ushahidi kwamba wanaume hutatizwa zaidi ya mafua ya kawaida na si kwamba huwa wanajifanya kwamba wamezidiwa.

Mtafiti mkuu Dkt Kyle Sue amesema wanaume huenda wana mfumo dhaifu kidogo wa kinga mwilini dhidi ya virusi vinavyosababisha mafua wakilinganishwa na wanawake.

Utafiti: Upara na nywele za kijivu ni ishara za magonjwa ya moyo

Wanaume wanaokuwa na upara kichwani mbali na wale wenye nywele za rangi ya kijivu wako katika hatari kubwa ya kupatikana na magonjwa ya moyo miongoni mwa wanaume walio chini ya umri wa miaka 40, utafiti unasema.

Utafiti uliofanyiwa zaidi ya vijana 2000 nchini India ulionyesha kuwa wengi waliokuwa na ugonjwa wa moyo walikuwa na upara na nywele za kijivu ikilinganishwa na wanaume walio na nywele kichwani.

Utafiti huo wa Idara ya magonjwa ya moyo barani Ulaya utasomwa katika kongamano la kila mwaka la magonjwa ya moyo nchini India.

Lakini wakfu wa Uingereza unaosimamia magonjwa ya moyo umesema kuwa sababu nyengine hatari pia ni muhimu.

Utafiti: Ngono haichangii sana mshutuko wa moyo

Image caption Ngono

Mshutuko wa ghafla wa moyo unaotokana na tendo la ngono unaweza kutokea zaidi miongoni mwa wanaume kuliko kwa wanawake, kwa mujibu wa utafiti.

Lakini hata hivyo pia kuna uwezekano mdogo kwa ngono kusababisha mshutuko wa moyo

Ni asilimia 34 ya visa 4,557 vya mshutuko wa moyo vilivytokea wakati wa tendo la au baada ya saa moja ya ngono na 32 kati ya wale walioathiriwa walikuwa ni wanaume.

Dr Sumeet Chugh, kutoka taasisi ya moyo ya Cedars-Sinai, anasema utafiti huo ndio wa kwanza kubaini ikiwa tendo la ngono linaweza kusababisha mshtuko wa moyo.

Utafiti: Ni hatari kwa wajawazito kulalia migongo yao

Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.

Utafiti wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito.

Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto.

Kondoo si wapumbavu sana, utafiti wabaini

Kondoo wamedhihirisha kwamba wana uwezo wa kutambua na kutofautisha nyuso za watu wanaowafahamu, kwa mujibu wa utafiti.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Cambridge waliweza kuwafundisha kondoo kutambua nyuso za watu mashuhuri wakiwemo waigizaji Jake Gyllenhaal na Emma Watson, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na mtangazaji wa BBC Fiona Bruce.

Baada ya mafunzo, kondoo walionekana kuchagua picha za nyuso walizozifahamu awali mara nyingi.

Utafiti: Jeraha la mchana hupona haraka kuliko lile la usiku

Wanasayansi nchini Uingereza wamegundua kwamba majeraha ya kukatwa na kuchomeka hupona haraka yanapopatikana mchana ikilinganishwa usiku.

Wanasema kwamba ni kutokana na mwili unavyohisi kulingana na muda.

Utafiti huo unasema kuwa seli za ngozi ya mwanadamu hubadilisha tabia yake kulingana na muda huku protini zinazohitajika kurekebisha majeraha hayo zikifanya kazi vizuri wakati wa mchana.

Utafiti: Mbwa mwitu hufanya uamuzi kwa kupiga chafya

Mbwa mwitu hufanya maamuzi yao kwa kupiga kura kupitia kupiga chafya kwa mujibu wa utafiti mpya.

Utafiti huo wa pamoja uliofanywa na wasomi kutoka Swansea, Australia na Marekani ulifuatilia mbwa mwitu walio kwenye hatari ya kuangamia nchini Botswana.

Watu wanaokunywa kahawa wanaishi miaka mingi: Utafiti

Ukikunywa vikombe vitatu vya kahawa kwa siku unaweza kuishi miaka mingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa karibu watu nusu milioni kutoka nchi 10 za Ulaya.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida na Annals of Internal Medicine, unasema kuwa unywaji wa kahawa unaweza kuongeza maisha ya mtu.

Familia yenye watu wasiohisi maumivu

Letizia Marsili, mwenye umri wa miaka 52, alitambua kwamba yuko tofauti kwa mara ya kwanza alipokuwa mdogo.

Hakuhisi maumivu kwa haraka, jambo linalomaanisha kwamba hakuhisi alipokuwa anateketea, au kutambua kwamba amevunjika mfupa mwilini. Jamaa zake watano pia katika familioa yao pia walikuwa katika hali hiyo na hawakuhisi maumivu.

Letizia ameiambia BBC: "siku hata siku tunaishi maisha ya kawaida, pengine maisha bora kuliko watu wengine, kwasababu ni aghalabu sisi kuwa wagonjwa, na hatuhisia maumivu.

"Hatahivyo, ki ukweli, maumivu yapo ila ni wa sekundi chache tu."

Utafiti: Watoto wanaozalishwa na wanaume wazee huwa werevu

Wanaume wanaochelewa kuanza familia wana uwezo wa kupata wavulana werevu kulingana na utafiti.

Watoto hao huwa werevu, wenye malengo kulingana na utafiti huo uliofanywa na chuo cha Kings College mjini London.

Umri wa mama huwa hauna athari yoyote na wasichana huwa na kinga.

Mwanasayansi mmoja anasema kuwa iwapo wanaume wataendelea kuchelewa kuanzisha familia basi tunaelekea katika jamii yenye watu werevu mno watakaoweza kusuluhisha matatizo duniani.

Utafiti: Umaarufu wa Magufuli washuka kwa asilimia 25

Umaarufu wa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli umeshuka kwa asilimia 25 kulingana na utafiti wa kura ya maoni iliofanywa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la Twaweza lililofanya kura hiyo Watanzania 7 kati ya kumi wanaunga mkono utendakazi wa rais Magufuli ikiwa ni sawa na asilimia 71 ikilinganishwa na asilimia 96 mwaka 2016.

Hatahivyo ripoti hiyo ya Twaweza inaonyesha kuwa rais Magufuli bado ana umaarufu miongoni mwa watu wazima walio na umri wa miaka 52 kuendelea kwa asilimia 82 huku wale ambao hawana elimu ya kutosha wakimuunga mkono kwa asilimia 75 huku walio maskini wakimuunga kwa asilimia 75.

Miongoni mwa vijana walio chini ya umri wa miaka 30, ni asilimia 68 pekee waliomuunga mkono, asilimia 63 wakiwa wasomi na asilimi 66 wakiwa matajiri.

Utafiti: Viwango vya mbegu za kiume vimepungua

Watafiti wanaochunguza matokeo yao tafiti 200 wanasema kuwa upungufu wa kiwango cha mbegu za kiume miongoni mwa Wanaume kutoka Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand ufikia nusu yake.

Baadhi ya wataalam wanashaka kuhusu matokeo hayo.

Lakini mtafiti bingwa anayeongoza utafiti huo Dkt Hagi Levine anasema kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika katika siku za usoni.

Dkt. Levine ambaye ni mtaalamu wa magonjwa aliambia BBC kwamba iwapo mwenendo huo utaendelea basi huenda binadamu wakatoweka.

Utafiti huo ambao ni miongoni mwa tafiti kubwa ulileta matokeo ya tafiti 185 kati ya 1973 na 2011.

Utafiti: Simu aina ya smartphone kudhibiti kisukari

Simu moja aina ya smartphone imechukuwa jukumu muhimu katika majaribio ambayo huenda yakawasaidia mamilioni ya watu duniani ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari kuweza kuthibti kiwango cha sukari.

Watafiti wa China katika jarida la sayansi wanasema walivumbua seli za insulini na kuzidunga ndani ya panya ili kufanya kazi wakati zinapoangazwa na mwanga wa LED.

Utafiti: Kerengende wa kike ''hujiuwa'' ili kukwepa tendo la ngono

Utafiti mpya umebaini kwamba kerengende wa kike huwa anajifanya kuwa amekufa ili kukwepa wenzao wa kiume.

Rassim Khelifa, kutoka chuo kikuu cha Zurich Switzerland, anasema kwamba aliona kerengende wa kike aliyekuwa akifuatwa na wa kiume ili kufanya mapenzi, akijiangusha na kulala kana kwamba amefariki, hadi pale kerengende wa kiume alipoondoka.

Ripoti hiyo imechapishwa kwenye jarida la ikolojia.

Bwana Khelifa amsema kuwa kerengende wa kike hunyanyaswa kwa sababu huwa hawana ulinzi baada ya kutaga mayai ikilinganishwa na kerengende wengine.

Utafiti: Unene wahusishwa na aina 11 za saratani

Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kwamba wamethibitisha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya kunenepa na aina kumi na moja za saratani.

Watafiti wamebaini kwamba unene unasababisha saratani kadhaa ikiwemo saratani ya tumbo, ini, matiti, utumbo na kizazi

Utafiti: Ndovu ndio mnyama anayelala kwa muda mfupi zaidi duniani

Wanasayansi waliowafuatilia ndovu wawili nchini Botswana wamebaini kuwa wanyama hao hulala muda mfupi zaidi ya mnyama mwengine yeyote duniani.

Ndovu hulala kwa saa mbili pekee hususan nyakati za usiku.

Wakiwa katika hifadhi, ndovu hulala kati ya masaa manne hadi sita kwa siku.

Utafiti: Betri zinazotumiwa katika simu zina sumu

Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya.

Utafiti huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium, ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.

Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.