Mwanamke ashangazwa na bili ya umeme ya dola bilioni 284

An electricity bill. File photo
Image caption Mwanamke ashangazwa na bili ya umeme ya dola bilioni 284

Bili ya umeme ya zaidi ya dola bilioni 284 ilimshangaza mwanamke mmoja katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani hadi alipogundua kuwa bili hiyo ilikuwa na makosa.

Mary Horomanski kutoka Erie, alisema kuwa bili hiyo ilionyesha kuwa alihitajika kulipa pesa hizo zote ifikapo Novemba mwaka 2018.

Kampuni ya umeme baadaye ilisema kuwa bili sahihi ilikuwa dola 284.46.

Msemaji wa kampuni alisema kuwa hawakufahamu jinsi hitilafu hiyo ilitokea ikionyesha kuwa Bi Horomanski alihitajika kulipa $284,460,000,000 huku akitakiwa kulipa sehemu ya kwanza ya dola 28,176 mwisho wa mwezi huu.

"Sijawi kuona bili ya mabilioni ya pesa," Mark Durbin aliliambia gazeti la Erie Times.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii