Afrika 2017: Habari zilizostaajabisha

This file photo taken on November 18, 2017 shows supporters of Tajamuka Sesijikisile SA, The African Democrats Opposition Party, the Zimbabwe Communist Party, the Zimbabwe Diaspora Coalition and other groups attending a rally at the Union Buildings in Pretoria, South Africa, to call for the resignation of Zimbabwe"s President. Haki miliki ya picha AFP

Matukio mengi ya kukumbukwa yalitokea mwaka 2017 yakiwemo kujiuzulu kwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mabadiliko sambamba katika nchi za Gambia na Angola.

Isisahaulike kufutwa kwa uchaguzi wa rais nchini Kenya ,kitendo kilichofanyika kwa mara ya kwanza Afrika.

Pia tumeripoti kuhusu majanga na ubunifu - lakini hizi ni baadhi ya habari za kushangaza kwa mwaka 2017.

'Githeri Man'

Mwanaume mmoja Mkenya aliyepigwa picha akitafuna 'githeri' chakula cha mahindi na maharagwe, wakati wa uchaguzi, alijipatia umaarufu mkubwa.

Image caption Mwanaume huyu ambaye aliongolewa sana na vyomvo vya habari Kenya

Githeriman, ambaye kwa jina lake halisi anaitwa Martin Kamotho, alivuma wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya tarehe nane mwezi wa nane alipoonekana kwenye mitandao ya kijamii akila chakula cha maharagwe na mahindi yakiwa ndani ya mfuko wake wa plastiki.

Bw Kamotho anajulikana sana kama "Githeri Man" alivuma sana kwenye mitandao ya jamii;

Makampuni makubwa kama vile Safaricom na Maisha Flour Milla yamejitokeza kumsaidia Githeriman na hivi sasa akaunti yake benki imeshiba kutokana na cheki alizoandikiwa na kampuni hizo.

Bw.Kamotho alikuwa miongoni ya wananchi 59 waliotunukiwa nishani za heshima na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe za kuidhinisha sikukuu ya jamhuri kwa sababu ya kazi walioifanyia nchi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, tuzo hiyo ni kwa minajili ya watu ambao "wameonesha uwezo wa hali ya juu, katika uongozi,ujasiri na uzalendo"

Hata hivyo baadhi ya Wakenya bado wanapata shida kufahamu ni nini hasa Bwana Kamotho alichofanya ili kupata heshima hiyo.

Dk. Shika wa milioni 900

Mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi,ulioharibika nchini Tanzania, iligeuka kumpatia umaarufu mwanaume mmoja kwa jina la Dk. Louis Shika .

Dk Shika alijizolea umaarufu baada ya kuibuka kwenye mnada huo na kutaja viwango vya juu vya fedha kuwapiku watu wengine waliojaribu kununua nyumba hizo.

Haki miliki ya picha IPP MEDIA
Image caption Dk Shika aliwashangaza wengi kwa mavazi yake ya kawaida mbazo hazikumuonesha kama mtu ambaye angeweza nunua nyumba za dola za Marekani milion 15 (Sh bilioni 3.2)

Lakini baada ya kutolipa asilimia 25 ya fedha zilizohitajika, alikamatwa na polisi kwa shutuma za kuharibu mnada,na kuachiwa baada ya kulipa dhamana.

Kwa mujibu ya vyombo vya habari nchini humo, kauli zake katika mnada huo, hasa ya '900 itapendeza' ,ndizo zilizompa umaarufu kiasi cha kupata udhamini wa kampuni tofauti.

Baada ya hapo maswali mengi yalivuma kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu ukweli wa hali yake Dk Shika,ambazo zinadai kwamba alikuwa mjasusi wa intelijinsia wa Marekani, CIA, anamiliki mabilioni ya fedha nchini Urusi na Uhispania.

Lakini pia ikatokea nafasi ya wengi kutania kuhusu sakata hilo;

Haki miliki ya picha JOTI/YOUTUBE
Image caption Msanii maarufu wa Tanzania, Joti, alimtania Dk Shika

"Polisi Kinyozi" aliyewaibisha wanawake

Mwezi Aprili, taasisi ya usalama barabarani Nigeria, walimuadhibu kamanda aliyepigwa video akiwaadhibu wafanyakazi wa kike kwa kuwakata nywele zao ndefu.

Picha zilimuonesha komanda huyo akitumia mkasi kuwakata nywele wakati wa ukaguzi na kuzua hisia za hasira mtandaoni.

Inasemekana kuwa wanawake hao walikuwa wamevunja kanuni za mitindo za nywele inayoruhusiwa na taasisi ya usalama barabarani (FRSC)

Haki miliki ya picha FRSC Rivers State/Facebook
Image caption Mwanaume mwenye kofia nyekundu akimkata nywele mwanamke hadharani

Msemaji wa FRSC alisema kitendo cha afisa huyo kilikuwa nje ya udhamini wa taasisi hiyo.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa jamii wa Twitter , Lauretta Onochie, msaidizi wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alikemea kitendo hicho na kukiita "udhalilishaji wa wanawake"

Kanisa la Walevi

Kanisa jipya nchini Afrika ya Kusini lilifungua milango yao na kuwakaribisha wavuta sigara na wanywaji pombe , ambao kwa kawaida hawapatiwi nafasi katika makanisa ya walokole.

Mtandao wa Habari Afrika Kusini ya eNCA, iliripoti kuwa, kanisa la Gobola mjini Johannesburg liliwakaribisha makundi ya watu na chupa za bia wakati wa ibada.

Askofu wa kanisa hilo, Tsietsi Matiki alisema kanisa ni "sehemu mwafaka" kwa wanywaji pombe na wavutaji sigara.

Lakini, eNCA wanaeleza , baraza la makanisa Afrika Kusini limelipinga kanisa hilo mpya.

Kwa mujibu wa mshiriki mmoja wa kanisa la Gobola, pombe inapewa tu kwa waumini waliona umri wa miaka 20 kwenda juu.

Vipara Msumbiji Walengwa

Mwezi Juni , polisi nchini Msumbiji walionya kuwa wanaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi yanayohusiana na uchawi.

Watu wanaamini kwamba mwili wa mtu mwenye kipara una dhahabu , kulingana na kamanda mmoja wa polisi kwa jina Afonso Dias aliiambia BBC mnamo mwezi Juni baada ya misururu ya mauaji yaliyolenga watu wenye vipara.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Baadhi ya raia nchini Msumbiji wanaamini kwamba mtu mwenye kipara ana dhahabu

Watu watano waliuwauwa wakati tuliporipoti habri hiyo.

Polisi pia waliwakamata watuhumiwa wawili walioshiriki katika mauaji hayo ya uchawi.

Soma zaidi hapa na hapa

Wabunge watwangana makonde Uganda

Wabunge nchini Uganda walipigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo

Wabunge wa upinzani wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa ni njama za kumuandilia njia Rais Yowei Museveni, mwenye miaka 73, kugombea tena mwaka 2021.

Katika kanuni za Katiba, mtu anayewania urais haruhusiwi kuwa na umri zaidi ya miaka 75.

Huwezi kusikiliza tena
Wabunge nchini Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge

Upande wa Afrika Kusini pia, mzozo huo huo ulitokea mwezi Februari, wakati wabunge wa upinzani wa Economic Freedom Fighters(EFF) walipigana na maafisa wa usalama baada ya wabunge hao kutosikiliza wito wa kutouvuruga hotuba ya taifa ya Rais Jacob Zuma.

Vurugu ilitokea kati ya wabunge na maafisa hao, ambao hatimaye walifanikiwa kuwatoa wabunge.

Suruali ni Marufuku Sudan

Polisi nchini Sudan walivamia sherehe katika mji mkuu wa Khartoum mwezi Disemba na kuwakuta wanawake wakivaa suruali.

Wanawake 24 walikamatwa na kushtakiwa kwa kutokuwa na maadili lakini baadaye mashtaka hayo yalifutwa.

Shambulio hiyo ilifanywa na idara ya poilisi yenye mamlaka ya kulinda maadili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanawake wa Sudan wakiwa Khartoum

Kama wanawake hao wangehukumiwa, wangepata adhabu ya mijeledi 40 na kutozwa faini.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wanakamtwa na kupigwa kwa "kuvaa nguo zisizo na maadili" kila mwaka na kuichapwa mijeledi.

Wanasema sheria inayopiga marufuku kuvaa suruali, sketi fupi au ya kubana katika nchi ambayo wengi ni Waislamu, ni ubaguzi dhidi ya Wakristo.

Kitamaduni, wanawake wa Sudan wanavaa nguo ndefu zisizobana kama baibui.

Soma zaidi hapa

#WengerOut

Maneja wa timu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenge anaendelea kuwagawana mashabiki wa klabu ya Arsenal, barani Afrika na kwengineko.

Mwezi Novemba, wakati Wazimbabwe wengi walikuwa wanatafakari kuhusu jeshi kuchukua mamlaka na maandamano katika mji mkuu wa Harare yaliotaka kumtoa Robert Mugabe mamlakani, wengineyo walichukua muda wao kudai Wenger aachie madaraka.

Maada hio ilionekana kuvuma mwaka huu. Picha hapo juu ikionesha maneno "Wenger Out" yaani "Wenger Toka" katika mechi ya soka nchini Ethiopia , siku mbili tu baada ya Arsenal kupoteza mechi dhidi ya Crystal Palace.

Maneno hayo pia yalionekana kwenye tamasha la muziki Kenya:

"Shahidi Bingwa'

Mkenya mmoja amewashangaza weni kwa siku nyingi baada ya kuto shuhuda ya ajali mbili zilizotokea katika maeneo tofauti nchini humo.

Picha ya mwanaume huyo alipotokea kwenye vyombo vya habari zilisambazwa sana katika mitandao ya jamii.

Mwanaume huyo aliyejitambulisha kama Dennis Muigai alihojiwa na kituo ch habari, Citizen TV baada ya ajali ya helikopta iliyowaua watu watano, tarehe 21 mwezi Oktoba.

Na kwa mara nyingine akawashahidi mkuu wakati ajali nyingine iliyotokea mwezi Novemba tarehe 7,huko Murang'a katikati mwa nchi. Ajali hio ilikuwa kilomita 200 kutoka ajali ya kwanza, ambapo gavana wa wa Nyeri alifariki.

Aliwaambia kituo cha televisheni, NTV, kuwa alikuwa abiria kwenye gari la polisi wakati ajali hio ilipotokea na akaelezea yaliyotokea kwa undani.

Kwa mujibu ya vyombo vya habari vya Kenya, baadaye polisi walikamata kwa shutuma za kumuiga afisa wa polisi,haujulikani nini ilimtokea baada ya hapo.

Baada ya yeye kuonekana televisheni, akageuka kuwa mada ya utani, na Wakenya wakaanza mada ya '#WitnessChallenge' kumuiga jinsi ambavyo alivyokuwa pamoja na miwani yake:

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii