Mauaji ya Benazir Bhutto: Ukweli uliofichwa na serikali ya Pakistan

Benazir Bhutto katika eneo la kampeni ya uchaguzi muda mfupi kabla ya kuuawa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Benazir Bhutto katika eneo la kampeni ya uchaguzi muda mfupi kabla ya kuuawa

Benazir Bhutto alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la Kiislamu .

Muongo mmoja baada ya mauaji yake umebaini yalioendelea Pakistan zaidi ikiwa kuusu aliyeagiza njama za mauaji yake.

Bhutto aliuawa mnamo tarehe 27 Disemba 2007 na mlipuaji wa kujitolea muhanga mwenye umri wa miaka 15 kwa jina Bilal.

Alikuwa amemaliza kampeni zake za uchaguzi katika mkutano wa kisiasa katika eneo la Rawalpindi wakati alipokaribia msafara wake akampiga risasi na kujilipua .

Bilal aliagizwa kutekeleza shambulio hilo na kundi la wapiganaji la Pakistan Taliban.

Benazir Bhutto alikuwa mwanawe wa kike Zulfikar Ali Bhutto , waziri mkuu wa kwanza Pakistan aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia .

Uongozi wake ulimalizwa baada ya kunyongwa na utawala wa kijeshi wa jenerali Zia-ulHaq. Benazir aliendelea na kuwa waziri mkuu mara mbili 1990, lakini hakuaminiwa na jeshi ambalo lilitumia madai ya ufisadi kumuondoa madarakani.

Wakati wa kifo chake, alikuwa akijiandaa kuwania muhula wa tatu kama waziri mkuu. Mauaji yake yalisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Pakistan.

Wafuasi wa Bhutto walifanya maandamano na kufunga barabara na kuwasha moto huku wakiimba nyimbo za kupinga mauaji ya kiongozi wao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shambulio hilo lilitokea sekunde chache baada ya picha yake kupigwa.

Jenerali na simu ya kutishia.

Muongo mmoja baadaye ,jenerali aliyekuwa akisimamia Pakistan wakati huo alikuwa amependekeza kwamba kuna watu katika utawala wake ambao walihusika na mauaji hayo.

Alipoulizwa iwapo kuna watu wabaya walioshirikiana na Taliban kuhusu mauaji hayo , Jenerali Pervez Musharraf alijibu: kuna uwezekano. Kweli. Kwa sababu jamii imegawanyika katika misingi ya kidini.

Na alisema watu hao huenda walihusika na mauaji yake. Ni taarifa ya kutatanisha kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Pakistan .

Kawaida viongozi wa jeshi nchini Pakistan hukana madai yoyote kuhusu maoni ya ushirikiano wa serikali katika mashambulizi ya kijeshi ya jihadi.

Image caption Pervez Musharraf alikana kumtishia Bhutto katika simu

Alipoulizwa iwapo alikuwa na habari fulani kuhusu watu serikali anaodai huenda walihusika katika mauaji hayo, alisema: Sina ushahidi wowote.

Lakini maoni yangu ni wazi.. nadhani mwanamke anayeonekana kulemea upande wa mataifa ya magharibi huchukiwa sana na watu kama hao.

Musharraf yeye mwenyewe alishatakiwa kwa mauaji, kuhusika katika vitendo vya uhalifu kwa lengo la mauaji mbali na kusaidia kutekeleza mauaji kuhusiana na kesi ya Bhutto.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa alimpigia simu Benazir Bhutto mjini Washinton tarehe 25 Septemba , wiki tatu kabla ya kukamilisha maficho yake ya miaka minane.

Msaidizi wa muda mrefu wa Bhutto Mark Seighal na mwandishi Ron Suskind wote wanasema waliandamana na Bhutto wakati simu hiyo ilipopigwa kulingana na Seighal muda mfupi baada ya simu hiyo.

Bhutto alisema: alinitishia. Aliniambia nisirudi, alinionya nisirudi. Musharraf alisema kuwa hatawajibika na kitakachomfanyikia Bhutto iwapo atarudi, Seighal aliambia BBC.

Na alisema kuwa usalama wake utategemea uhusiano wao. Musharraf amekana kupiga simu hiyo na kupinga wazo kwamba huenda aliagiza mauaji yake.

Kwa kweli nilicheka, aliambia BBC hivi karibuni..Kwa nini nimuue?

Njama kali

Kesi dhidi ya Musharraf imekwama kwa sababu alitorokea mafichoni mjini Dubai.

Mwana wa Benazir Bhutto ambaye amemrithi mamake kisiasa Bilawal amekana matamshi ya Musharraf.

Musharraf alitumia kila njia ili kumuua mamangu, alisema. Kwa makusudi alihujumu usalama wake ili auawe na kuondolewa katika eneo la muaji.

Haki miliki ya picha Dawn News TV
Image caption Mshambuliaji alimpiga risasi kabla ya kujilipua
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alimpiga risasi Bhutto kabla ya mlipuko kutokea.

Huku kesi ya Musharraf ikiwa imekwama , wengine wameachiliwa kwa kutenda uhalifu huo .

Katika wiki chache za mauaji hayo washukiwa watano walikiri kumsaidia kijana huyo wa miaka 15 Billal kumuua Bhutto kutokana na maagizo ya kundi la Taliban la Pakistan na lile la al-Qaeda.

Mtu wa kwanza kukamatwa , Aitzaz Shah, aliambiwa na kundi la Taliban la Pakistan kwamba ndiye atakayekuwa mlipuaji wa kujitolea aliyechaguliwa kumuua Bhutto.

Lakini baadaye akawekwa kama mlipuaji wa ziada iwapo jaribio la shambulio hilo litafeli.

Washukiwa wengine wawili Rasheed Ahmed na Sher Zaman , walikiri walikuwa wakipanga njama hiyo pamoja na binamu wao wawili katika eneo la Rawalpindi Hasnain Gul na Rafaqat Husain.

Waliambia mamlaka kwamba walitoa nyumba ya kulala ya Bilal usiku kabla ya mauaji hayo.

Haki miliki ya picha AFP
Haki miliki ya picha AFP

Hata iwapo ushahidi huo ulifutiliwa mbali , rekodi za simu zilionyesha maeneo ya washukiwa hao pamoja na mawasiliano yao saa chache kabla ya mauaji ya bi Bhutto .

Hasnain Gul aliwapeleka maafisa wa polisi na kuonyesha ushahidi katika nyumba aliokuwa akiishi.

Chembechembe za DNA kutoka mwili wa Bilal uliokusanywa baada ya shambulio hilo kabla ya kupimwa katika maabara zilithibitisha chembechembe kama hizo katika viatu vya mazoezi, kofia, na nguo ambayo Bilal alikuwa ameiwacha nyuma katika makaazi ya Husnain wakati alipovaa vesti ya kujilipua,

Image caption Watu watano wanaodaiwa kupanga njama ya mauaji hayo walikamatwa mapema mwaka huu na polisi

Miezi michache iliopita , waendesha mashtaka walikuwa wanaamini kwamba watu hao watapatikana na hatia.

Lakini mnamo mwezi Septemba kesi hiyo ilianguka , huku jaji akitangaza kwamba kulikuwa na makosa kuhusu vile ushahidi ulivyokusanywa na kuwasilishwa mahakamani, hatua iliomlazimu kuwaachilia huru.

Watano hao bado wanaendelea kuzuiliwa huku rufaa ikitarajiwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Benazir Bhutto katika eneo la kampeni ya uchaguzi muda mfupi kabla ya kuuawa

Benazir Bhutto alikuwa nani?

Haki miliki ya picha AFP

Ni mtu aliyetawala siasa za Pakistani ,Bi Bhutto alihudumu mara mbili kama waziri mkuu wa taifa hilo kutoka 1988 hadi 1990 na kutoka 1993 hadi 1996.

Akionekana kuwa mwenye umri mdogo na kupendeza , alifanikiwa kujionyesha kuwa mtu aliyeleta uongozi mpya ikilinganishwa na siasa za taifa hilo zilizotawaliwa na wanaume.

Lakini baada ya kuondolewa madarakani kwa mara ya pili , alishirikishwa na ufisadi na uongozi mbaya.

Bi Bhutto aliondoka Pakistan 1999 lakini akarudi 2007 baada ya rais aliyekuweko madarakani Musharraf kudai kwamba yeye na wengine hawakuhusika na maswala ya ufisadi.

Alitarajiwa kushiriki katika uchaguzi ulioitishwa na bwana Musharraf mnamo mwezi Januari 2008. Lakini msafara wake wa kurudi nyumbani mjini Karachi ulilipuliwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga miezi miwili baadaye

Haki miliki ya picha AFP

Mumewe aliyekuwa rais

Nchini Pakistan, ni swala la kawaida kusikia watu wa kawaida wakimshutumu mumewe Bhutto Asif Zardari kwa kupanga njama ya mauaji hayo.

Madai hayo ni ya kawaida kutokana na imani kwamba baada ya kifo cha mkewe ni yeye aliyefaidi.

Mbinu hiyo hatahivyo haijatoa ushahidi hata mmoja kuonyesha kwamba Asif Zardari alihusika kwa njia yoyote ile kwa kifo cha mkewe.

Amekana madai hayo, na kuongeea kuwa wale wanaoleta madai kama hayo wanafaa kunyamaza.

Image caption Azif Zardari amesema kuwa wale ambao hawajasikia uchungu alionao wanafaa kunyamaza

Asif Zardari anakabiliwa na madai mengine : kwamba licha ya kuwa na uwezo wa rais alishindwa kuchunguza vizuri mauaji ya mkewe .

Nakala za siri zinazohusiana na uchunguzi na zilizopatikana na BBC zinaonyesha kuwa uchunguzi wa polisi ulifanywa vibaya hatua iliothibitisha kuwa hawakutaka kuwapata watu wengine na hatia zaidi ya wale iliowakamata.

Mapungufu ya uchunguzi wa polisi yalionekana baada ya jaribio ambalo halikufanikiwa kuhusu maisha ya Bhutto mnamo tarehe 18 Oktoba 2007 -miezi miwili na nusu kabla ya kuuawa.

Walipuaji wawili wa kujitolea muhanga walishambulia msafara wake na kuwaua zaidi ya watu 150 .

Ni miongoni mwa mauaji mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na Wanajihad nchini Pakistan.

Maafisa wa polisi walishindwa kutekeleza uchunguzi mzuri na kwamba hata walioshambulia pia hawakupatikana. kiongozi wa uchunguzi huo Saud Mirza , alisema kuwa mtu mmoja ambaye alimtambua kuwa mshambuliaji alikuwa na vitu vinavyoonyesha kuwa alitoka katika jamii ndogo mjini Karachi iliokuwa na asili ya Kiafrika.

Hatahivyo viasharia hivyo kuhusu mlipuaji huyo havikutolewa kwa umma. Aliyekuwa rais Zardari aliwajibu wakoasoaji wake kuhusu uchunguzi huo wa polisi akisema kuwa alishirikiuha maafisa wa ujasusi wa Uskochi mbali na kuanzisha uchunguzi uliofanywa na tume ya Umoja wa mataifa.

Uchunguzi huo hatahivyo ulidaiwa kuzuiliwa sio na jeshi pekee bali hata mawaziri wa rais Zardari. Kulikuwa na watu wengi katika utawala huo ambao ulitaka kuwachunguza lakini walikataa, alisema Heraldo Munoz, kiongozi wa tume hiyo ya UN.

Na Alisema kuwa baadhi ya vikwazo vilitoka kutoka kwa wanasiasa pamoja na wanajeshi. Huku uchunguzi ukiendelea, alisema nyumba salama iliokuwa ikitumiwa na UN ilichukuliwa mbali na maafisa wa kukabiliana na ugaidi waliokuwa wakiwalinda maafisa wa UN.

Msururu wa watu waliofariki...

Kwamba uchunguzi wa kifo hicho ulifichwa hakuna shaka.

Uchunguzi wa BBC ulibaini ushahidi ulioonyesha kuwa watu wawili waliomsaidia muuaji aliyejilipua kumfikia Benazir Bhutto walipigwa risasi katika kizuizi kimoja cha jeshi tarehe 15 Januari 2008 .

Afisa mmoja mkuu wa serikali ya Zardari aliambia BBC kwamba anaamini kwamba huo ulikuwa mpango wa kuzuia uchunguzi -Neno linalotumika na raia wa Pakistan kwa mauaji ya kiholela.

Nadir na Nasrulla Khan walikuwa wanafunzi wa Taliban waliokuwa wakiunga mkono Madrassa ya Haqqania kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Wanafunzi wengine waliohusishwa na madrassa hiyo ambao pia walikuwa katika njama hiyo walifariki.

Nakala yenye maelezo zaidi iliopatikana na BBC iliwasilishwa katika bunge la mkoa la Sindh. Imetaja majina ya Abad ur Rehman, mwanafunzi wa zamani katika madrassa hiyo na mtengenezaji wa bomu kuwa watu waliosaidia kupatikana kwa vesti ya vilipuzi iliotumika kumuua Benazir Bhutto.

Aliuawa katika eneo moja la mashambani nchini Pakistan mnamo tarehe 13 mwezi Mei 2010. Baadaye kulikuwa na Abdullah ambaye kulingana na ripoti hiyo iliowasilishwa katika bunge la Sindh alihusika na usafirishaji wa vesti hiyo kabla ya kufanyika kwa mauaji hayo. Kifo cha mlinzi wake Khalid Shahenshah.

Shahenshah hakuwa mbali na Bhutto wakati alipokuwa akitoa hotuba yake mjini Rawalpindi.

Rekodi za mawasiliano ya simu zimeonyesha kuwa alifanya safari zisizo za kawaida ambazo hakuna mtu aliyeweza kutoa sababu yake.

Ijapokuwa hakuonyesha ishara zozote alionekana akimwangalia Bhutto kwa macho makali huku akijaribu kumshika shingo yake.

Picha za kitendo chake zilisambazwa na mnamo tarehe 22 mwezi Julai 2008, Shahenshah alipigwa risasi nje ya nyumba yake mjini Karachi.

Mwathiriwa mwengine ni mwendesha mashtaka wa serikali The next victim was the state prosecutor, Chaudhry Zulfikar. Akiwa wakili mwenye sifa nyingi aliwaambia marafikize kwamba anaendelea vyema na uchunguzi wa Bhutto.

Haki miliki ya picha FAROOQ NAEEM
Image caption Mwendesha mashtaka maalum wa serikali Chaudhry Zulfiqar Ali aliuawa katika mji mkuu

Mnamo tarehe 3 mwezi Mei 2013 alipigwa risasi barabarani mjini Islamabad alipokuwa akipelekwa katika kesi moja

... na mtu aliyedaiwa kuwa amefariki lakini akabainika alikuwa hai

Hatimaye kulikuwa na mtu aliyedaiwa kuwa amefariki , lakini ukweli ni kwmba alikuwa hai. katika ushahidi wao, wapanagaji wa mauaji hayo walisema kwamba katika siku ya mauaji mlipuaji mwengine wa pili kwa jina Ikramullah aliandamana na Bilal.

Baada ya Bilal kufanikiwa katika jukumu lake ,huduma za Ikramullah hazikuhitajika na aliondoka bila kuumizwa

Miaka kadhaa baadaye maafisa wa Pakistani walisisitiza kuwa Ikramullah aliuawa katika shambulio la ndege isiokuwa na rubani.

Mwaka 2017 mwendesha mashtaka Mohammad Azhar Chaudhry aliambia BBC kwamba ushahidi uliopatikana kutoka kwa vitengo vya uchunguzi vya Pakistan ulithibitisha kuwa "Ikramullah alikuwa amefariki''.

Mnamo mwezi Agosti 2017, hatahivyo, mamlaka ya Pakistan ilichapisha kurasa 28 ya orodha ya magaidi wanaosakwa .

Katika nambari ya tisa ni Ikramullah, mkaazi wa kusini mwa Waziristan na alihusika katika mauaji ya Benazir Bhutto, orodha hiyo ilisema

BBC inaelewa kwamba Ikramullah sasa anaishi mashariki mwa Afghanistan ambapo amekuwa kamanda wa kadri wa Taliban nchini Pakistan.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauaji ya Bhutto yaliwaacha mashabiki wengi wa Bhutto na mshtuko.

Kufikia sasa ni maafisa wawili wa polisi pekee walioadhibiwa kuhusiana na mauaji hayo baada ya kuagiza eneo la mauaji hayo huko Rawalpindi kufungwa.

Raia wengi wa Pakistan wanahisi adhabu hiyo sio ya haki wakiamini kwamba maafisa wa polisi hawawezi kuchukua hatua hiyo bila agizo la jeshi.

Inaonyesha ukweli ulivyofichwa na serikali ya Pakistan-mbali na mtandao wa maafisa wa jeshi walioastaafu na wale wanaoendelea kuhudumu , wanaolinda maslahi ya kitaifa ya Pakistan.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii