Mama wa "maisha na kifo" ahukumiwa miaka 14 jela Bosnia

Azra Bašić is extradited from the US to extradited to the Prosecutor’s Office of Bosnia and Herzegovina, 22 November 2016 Haki miliki ya picha Bosnia State Prosecutor's Office
Image caption Mama wa "maisha na kifo" ahukumiwa miaka 14 jela Bosnia

Mahakama nchini Bosnia imemhukumu mwanamke mmoja anayefahamika kama "mama wa maisha na kifo" kifungo cha miaka 14 kufuatia uhalifu wa kivita uliotokea miaka tisini.

Azra Bašić alipatikana na hatia ya kuhusika kwenye uhalifu wa kivita wakati wa vita vya Balkan ikiwemo kuwatesa watu wa asilia ya Sebia.

Jaji alisema kuwa Bašić alihusika na kuteswa kwa watu waliokuwa wakizuiwa na vikosi vya Bosnia na Croatia.

Hukumu yake ndiyo kali zaidi kuwai kupewa mwanamke kutokana na uhalifu uliotokea wakati wa mzozo wa Bosnia.

Walioshuhudia walisema kuwa kuwa alichora misalaba kwa kuwakata nyuso wafungwa, akamlazimisha mwanamume mmoja kunywa petroni kabla ya kuwasha moto mikono yake na uso na kuwalazimisha watu walio uchi kutembea kwa tumbo zao ju la vioo vilivyovunjika.

Bašić amekuwa akiishi nchini Marekani akijutumia jina tofauti kwa karibu miaka 20 kabla ya kukamatwa mwaka 2011. Marafiki wanasema kuwa alikuwa na roho nzuri na mwenye tabia njema.

Takriban watu 100,000 kwa jumla waliuawa wakati wa vita vya Bosnia. Mzozo huo ulidumu kwa karibu miaka minne kabla ya makubaliano yaliyofanya na Marekani na kusababisha vita hivyo kumalizika mwaka 1995.

Mada zinazohusiana