Cameroon yamtimua mkosoaji mkubwa wa rais Paul Biya

Patrice Nganang Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Profesa Patrice Nganang

Jaji mmoja nchini Cameroon ametoa uamuzi wa kuachiliwa kwa muandishi anayeishi Marekani na msomi aliyekamatwa kwa madai ya kumtishia maisha rais Paul Biya.

Jaji huyo aliatoa uamuzi kwamba Patrice Nganang afurushwe kutoka jimbo la Afrika ya Kati, wakili wake amesema.

Hakuna sababu maalum iliyotolewa kwa uamuzi huo wa kumuachilia huru raia huyo wa Marekani.

Rais wa Cameroon aadhimisha miaka 35 uongozini

Mkosoaji mkubwa wa rais wa Cameroon ahukumiwa miaka 25 jela

Ulinzi waimarishwa Cameroon

Bw Nganang alikamatwa wiki tatu zilizopita alipokuwa akiondoka katika nchi yake ya kuzaliwa. Ni mkosoaji mkubwa wa Bw Biya kwa miaka 35 ambayo amekuwa uongozoni.

Serikali inamlaumu kwa kumtishia kumpiga risasi rais Biya kwenye chapisho lake la Facebook, madai yanayosemekana kuchapishwa baada yake kuzuru mataifa ya magharibi yanayozungumza Kiingereza hasa katika eneo linalotumia lugha ya Kifaransa ya Cameroon.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakereketwa wailamu serikali kwa kutumia nguvu kwa waandamanaji

Bw Nganang hakupatikana na hatia wakati alipokuwa mahakamani tarehe 15 Disemba.

Wakili wake, Emmanuel Simh , amesema kesi hiyo ''ilikuwa na misingi ya kisiasa'' dhidi ya mtu aliyekoa uongozi wa Bw Biya.

Bw Nganang ni professa wa fasihi kwenye chuo kikuu cha Stony Brook mjini New York.

Bw Nganang ni muandishi aliyeshindi tuzo ya vitabu vya riwaya ikiwemo ''Temps de Chien", ama "Dog Days" ambayo iliangazia maisha nchini Cameroon chini ya uongozi wa bw Biya.

Bw Nganang alipokonywa cheti cha usafiri na kukamatwa, alipokuwa akitaka kuabiri ndege kuelekea Zimbabwe.

Familia yake na marafiki wamesema alikuwa amekamatwa kwa kuandika taarifa kwa gazeti la Ufaransa la Jeune Afrique , akiiikashifu serikali ya Bw Biya jinsi inavyokabiliana na waandamaji na raia wa Cameroon ambao huzungumza Kiingereza.

Makumi waliuawa mwezi Novemba katika msako uliofanywa kwa waandamanaji.

Raia wengi ambao hutumia Kiingereza wanawalaumu wengi ambao hutumia lugha ya Kifaransa kwa ubaguzi.

Haki miliki ya picha Atlas
Image caption Ramani ya Cameroon

Wakisema hubaguliwa kwenye kazi za viwango vya juu za umma kutokana na sheria za kifaransa na mfumo wa kisheria kazi hizo zilizowekewa.

Serikali imekana madai hayo na kusisitiza kwamba inachukulia raia wote sawa.

Mgawanyiko katika mataifa ya kati ya Afrika ulianza wakati wa wakoloni walipokuwa wakijitafutia makazi

Cameroon ilikombolewa na Ujerumani na kugawanyika mara mbili ikiwa na upande wa Muingereza na Mfaransa baada ya vita ya kwanza vya Dunia.

Baada ya kura ya maoni, Waingereza ambao walikuwa wakitawala kusini mwa Cameroon waliungana na Jamhuri ya Cameroon iliyokuwa inatawaliwa na Mfaransa mwaka 1961

Kwa sasa Cameron imegawanyika katika maeneo ya Kusini Magharibi na Kaskazini Magharibi.

Matamanio ya kupata uhuru yameongezeka katika maeneo hayo mawili kwa miaka ya hivi majuzi na serikali imeapa kusitisha mashambulizi yanayolaumiwa kutoka kwa jeshi la serikali.

Mada zinazohusiana