Mwanamke anayekusanya nguo za waathiriwa wa ubakaji India

Jasmeen Patheja akionyesha nguo za waathiriwa wa ubakaji Haki miliki ya picha ASIF SAUD
Image caption Jasmeen Patheja akionyesha nguo za waathiriwa wa ubakaji

Msanii wa India Jasmeen Patheja amekuwa akikusanya nguo zinazotolewa kama msaada na waathiriwa wa ubakaji kama thibitisho si wakulaumiwa , mwanahabari wa BBC Geeta Pandey.

Katika chumba kidogo chenye nyumba yake ya kifahari ambayo imegeuzwa na kuwa nyumba ya makumbusho ya nguo. Nguo ambazo wanawake huzivaa kila mara , zina historia yake.

Huu ni mkusanyiko wa nguo za Jasmeen Patheja za watu walionajisiwa kijinsia. Nguo moja yenye rangi nyekundu na nyeusi ilitolewa kama msaada na mwanamke aliyebakwa wakati wa unyanyasaji mkubwa uliotokea katika sherehe za mkesha wa muamko wa mwaka mpya huko Bangalore mwaka uliopita.

''Amesema alikuwa katika sherehe hiyo ambapo kundi kubwa la watu walianza kuwapapasa wanawake, Bi Pantheja amesema. ''amezungumzia jinsi alivyonyanyaswa alipokuwa akitafuta uhifadhi.''

Halafu akashika nguo nyengine ya rangi ya malai Kurta, na maua ya rangi nyeusi na nyekundu- nguo ambayo inavutia. Ilitolewa na mwanamke aliyepapaswa akiwa safarini kwenye treni kusini mwa mji wa Coimbatore.

Haki miliki ya picha ASIF SAUD
Image caption Chumba cha maonyesho kwenye nyumba ya Patheja

''Aliniambia alikatazwa kuripoti kisa hicho cha unyanyasaji.''

Rinda lenye rangi ya waridi ambalo ananionyesha lilitoka kutoka kwa mwanamke mmoja Montreal. ''alisema iwapo hutachukua rinda hilo , angeiltupa.

Na lilimfanya kuugua zaidi alipokuwa na rinda hilo, bi Patheja amesema.

Tukizidi kuangalia sanduku la nguo akanionyesha rinda jeupe , nguo ya kuogelea , kaptula, sare za shule - mfano alioueleza kama ''Kioo'' kudhihirisha kwamba wanawake hupitia unyanyasaji wa kijinsia.

''Haina uhusiano wowote na kile mtu anachokivaa, hakuna sababu yoyote ya kunajisiwa na hakuna ambaye hutaka kunajisiwa.''

Na ndio sababu mradi wake unaitwa- 'I never Ask For It''

''Mradi huo unataka kutoa nafasi ya kuhifadhi habari mbaya za uchungu na uoga''

Haki miliki ya picha ASIF SAUD
Image caption Baadhi ya nguo

Patheja, alianza kupigana dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia karibu muongo mmoja na nusu uliyopita , baada ya kuhamia Bangalore kutoka Kaskazini mwa mji wa Kolkata kusomea somo la Sanaa.

''Sio kwamba hakuna visa vya unyanyasaji wa kijinsia katika mji wa Kolkata, lakini nilikuwa mgeni Bangalore.

Nilikuwa na miaka 23 na sikuwa na familia ya kukimbilia endapo ningetaka usaidizi,''alisema.

''Ilikuwa ni wakati ambapo unyanyasaji ulikuwa ukishuhudiwa barabarani na ukipuziliwa mbali kama ''kitu cha kawaida'' ambacho kijana au msichana anastahili kupitia.

''Ilikuwa imehalalishwa''. Kulikuwa na hali ya kulinyamazia swala hilo ambalo ilifanya jambo hilo kuendelea.''

Kama njia ya kukabiliana na kimya hicho, aliamua kuanza kulizungumzia .

Mada zinazohusiana