Shirika la ndege laomba wachezaji msamaha kwa kuwashuku kuiba blanketi

American Airlines Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption American Airlines

Shirika la American Airlines limewaomba msamaha wachezaji wawili wa mpira wa kikapu ambao walifukuzwa kutoka kwa ndege kwa kuwashuku kuiba.

Marquis Teague na Trahson Burrell waliabiri ndege hiyo siku moja kabla ya krismasi wakielekea kucheza mechi.

Lakini kabla ya ndeye kuondoka uwanjani, mhudumu mmoja wa ndege alidai kuwa wanaume hao walikuwa mablanketi kutoka upande wa kifahari wa ndege ambapo walilazimishwa kushuka kutoka kwe ndege hiyo.

Baadaye ilibainika kuwa ni abiria walikuwa wamewapa mablanketi hayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marquis Teague (kushoto) na Trahson Burrell (kulia) hawajasema lolote

Wachezaji hao wote walikuwa wa asilia ya Afrika akiwemo mhudumu wa ndege.

Hakuna mchezaji kati ya hao wanaochezea timu ya Memphis Hustle amezungumzia kisa hicho.

Laiki naibu kocha wa Hustle, Darnell Lazere aliandika katika twitter kuwa kitendo hicho kilichochewa na ubaguzi wa rangi.

Wachezaji walikuwa wakisafiri kutoka uwanja wa Dallas-Fort Worth kwenda Sioux Falls, South Dakota wakitumia ndege ya Envoy Air iliyo sehemu ya American Airlines.

Mada zinazohusiana