Kenya yapiga marufuku uvutaji wa shisha

Katika ilani ya gazeti rasmi la serikali , waziri wa Afya Cleopa Mailu amepiga marufuku uagizaji, utengenezaji utangazaji na uuzaji wa shisha nchini humo
Image caption Katika ilani ya gazeti rasmi la serikali , waziri wa Afya Cleopa Mailu amepiga marufuku uagizaji, utengenezaji utangazaji na uuzaji wa shisha nchini humo

Wizara ya afya nchini Kenya imepiga marufuku uvutaji wa shisha mara moja.

Katika ilani ya gazeti rasmi la serikali , waziri wa Afya Cleopa Mailu amepiga marufuku uagizaji, utengenezaji utangazaji na uuzaji wa shisha nchini humo.

Kenya sasa ni taifa la tatu kupiga marufuku shisha baada ya Tanzania na Rwanda katika eneo la Afrika mashariki.

Katika gazeti hilo la serikali la tarehe 28 mwezi Disemba, Dkt. Mailu alionya kuwa mtu yeyote atakayepatikana akikiuka sheria za udhibiti wa uvutaji wa shisha atapigwa faini isiopungua shilingi 50,000 za Kenya ama kifungo cha muda usiopungua miezi sita ama zote mbili.

Akithibitisha ilani ya gazeti rasmi la serikali, mkurugenzi wa huduma za matibabu Jackson Kioko alisema: Uamuzi wetu wa kuweka marufuku hiyo unatokana na sababu za kiafya na kijamii mbali na ushahidi wa kisayansi kuhusu madhara ya uvutaji wa Shisha.

Mataifa mengine ambayo yamepiga marufuku uvutaji wa Shisha ni Pakistan, Jordan, Singapore and Saudi Arabia.

Image caption Shisha hushirikisha bidhaa za tumbaku ambazo hutiwa ladha na huvutwa kwa kutumia mirija kadhaa ilio na maji ambayo moshi wake hupitia kabla ya kumfikia mvutaji.

Shisha hushirikisha bidhaa za tumbaku ambazo hutiwa ladha na huvutwa kwa kutumia mirija kadhaa ilio na maji ambayo moshi wake hupitia kabla ya kumfikia mvutaji.

Shirika la afya duniani hivi majuzi lilibaini kwamba uvutaji wa Shisha ni hatari kwa afya kwa sababu uvutaji wa sigara 100 ama hata zaidi hufanyika kwa awamu moja wakati mtu anapovuta shisha.

Nchini Tanzania uvutaji wa Shisha ulipigwa marufuku kutokana na wasiwasi kwamba unahusishwa na dawa za kulevya na pombe.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliripotiwa akisema kuwa uvutaji wa shisha una madhara makubwa kwa vizazi vijavyo

Mada zinazohusiana