Akaunti ya mwanzilishi wa McAfee VirusScan yadukuliwa

John McAfee amesema kuwa akaunti yake ya mtandao wa Twitter ilidukuliwa na kutumika kukuza sarafu zisizojulikana za crypto. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption John McAfee amesema kuwa akaunti yake ya mtandao wa Twitter ilidukuliwa na kutumika kukuza sarafu zisizo na umaarufu mkubwa za crypto.

John McAfee amesema kuwa akaunti yake ya mtandao wa Twitter ilidukuliwa na kutumika kukuza sarafu zisizo na umaarufu mkubwa za crypto.

Mtaalam huyo aliyeanzisha programu za usalama wa mtandaoni ameshutumu madai kwamba kisa hicho kinahujumu sifa zake akisema: Sina udhibti wa usalama wa Twitter.

Lakini alichapisha kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba simu yake ya rununu iliingiliwa.

Mtandao wa Twitter ulikataa kutoa tamko lolote lakini ukatoa ushauri kuhusu maelezo ya usalama wake.

Mtandao huo wa kijamii hutaka mtu kuingia kupitia kodi iliotumwa katika simu yake mbali na neno la siri ili kuzuia visa kama hivyo.

Bwana McFee aliambia BBC kwamba alianza kutumia maelezo hayo lakini akaongezea kuwa anaamini kwamba aliyemdukua aliingilia kati nambari inayotumwa katika simu.

Haki miliki ya picha MGT
Image caption Mgombea huyo wa zamani wa urais kwa sasa ameanza mipango ya kuuza simu aina ya smartphone ambayo haiwezi kudukuliwa.

Mgombea huyo wa zamani wa urais kwa sasa ameanza mipango ya kuuza simu aina ya smartphone ambayo haiwezi kudukuliwa.

Bwana McAfee alijipatia umaarufu 1980 wakati alipoanzisha kampuni iliotengeza programu ya kukabiliana na virusi katika kompyuta ya McAfee VirusScan - hatua iliomsaidia kumiliki kampuni kubwa yenye thamni ya mabilioni ya dola.

Ijapokuwa biashara hiyo baadaye aliiuza kwa kampuni ya Intel ,bado angali kutengeza bidhaa za kukabiliana na udukuzi wa mitandaoni.

Mada zinazohusiana