George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia

Mwanasoka maarufu George Weah ashinda urais Liberia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanasoka maarufu George Weah ashinda urais Liberia

George Weah Leo atatangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo baada ya kuongoza kwa asilimia 61.5 kati ya kura asilimia 98.1 zilizohesabiwa.

Bwana Weah amemtangulia mpinzani wake Joseph Boakai kwa kura asilimia 60.

Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia.

"Waliberia wenzangu, ninazielewa kwa undani hisia za watu wote wa taifa zima," Bw Weah aliandika kwenye Twitter baada ya matokeo kutangazwa.

"Ninaelewa umuhimu na majukumu ya kazi kubwa niliyokabidhiwa leo. Mabadiliko yanakuja."

George Weah ni nani?

Weah ni mwanasoka maarufu aliyecheza kwenye klabu za soka za juu Ulaya kama Paris St-Germain (PSG) na AC Milan, kabla ya kumaliza taaluma yake nchini Uingereza kwa kuwachezea kwa muda mfupi klabu za Chelsea na Manchester City.

Ni Mwafrika pekee aliyewahi kushinda tuzo ya Fifa ya mchezaji bora duniani ya na tuzo ya Ballon D'Or.

Aliingia katika uwanja wa siasa baada ya kustaafu kucheza mwaka 2002 na sasa ni seneta katika bunge la Liberia.

Tulifikaje hapa?

Liberia ni nchi iliyoanzishwa na watumwa waliopewa uhuru kutoka Marekani, lakini nchi hiyo haijawahi kuwa na mabadiliko rahisi ya madaraka tangu mwaka 1944.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption George Weah alishinda duru ya kwanza mwezi Oktoba

Bi Johnson Sirleaf alimshinda George Weah, katika uchaguzi wa mwaka 2005, na kuchukua madaraka mwaka uliyofuata baada ya kuisha kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopelekea Rais Charles Taylor kutolewa madarkani na waasi.

Taylor sasa amefungwa kwa miaka 50 nchini Uingereza baada ya kuhukumiwa kwa vitendo vya uhalifu nchini Sierra Leone.

Kampeni ya Bw Weah, chini ya muungano wa mabadiliko ya demokrasia, uliolenga kura ya vijana wakati mpinzani wake makamu wa rais Boakai alionekana kupitwa na wakati na kutokuwa na mashiko.

Lakini uchaguzi wa Weah haukwenda bila mvutano, kwa kuwa mgombea mwenza alikuwa Jewel Taylor mke wa zamani rais aliyefungwa Charles Taylor.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii