Watu 9 wauawa katika shambulio la kanisa Misri

Watatu ya waliouawa ni maafisa wa polisi waliokuwa katika zamu katika kanisa la Mar Mina. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watatu ya waliouawa ni maafisa wa polisi waliokuwa katika zamu katika kanisa la Mar Mina.

Watu tisa wamefariki baada ya washambuliaji waliojihami na bunduki walipojariubu kuvamia kanisa moja kusini mwa Cairo, lakini wakazuiliwa na maafisa, maafisa wanasema.

Watatu ya waliouawa ni maafisa wa polisi waliokuwa katika zamu katika kanisa la Mar Mina.

Mshambuliaji mmoja aliuawa na mshipi wake uliojaa vilipuzi kutibuliwa.

Mpiganaji mwengine alifanikiwa kutoroka.

Huduma za usalama zilitangaza mipango wiki hii ya kulinda sherehe wakati wa mwaka mpya na Krisimasi ya kanisa la Coptic.

Walipanga kupeleka kikosi cha kukabiliana na dharura.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wamisri wa kanisa la Coptic wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara

Shambulio hilo la siku ya Ijumaa lilifanyika wakati ambapo maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria nje ya kanisa hilo walikutana na watu wawili waliowashuku, kulingana na mwandishi wa BBC mjini Cairo Radwa Gamal.

Waliwakaribia watu hao wawili ambao walianza kwa kuwafyatulia risasi polisi hao.

Kuna ripoti kwamba watu kadhaa walijeruhiwa ,wawili vibaya.

Mada zinazohusiana