Wanaotumia vibaya fedha za kukabiliana na umasikini China kuadhibiwa

Ramani ya China
Image caption Ramani ya China

China imesema inawachukulia hatua kali wote watakaobainika kutumia vibaya fedha walizopewa kwa minajili wazitumie kijikwamua kutoka lindi la umaskini.

Kwenye orodha hiyo kuna majina ya raia 450 wanaosemekana kuzifuja fedha hizo -lakini haijabainika ni adhabu gani walizopewa.

Katika miaka ya hivi karibuni China imekuwa ikiendeleza mkakati wa kukabiliana na umaskini wa kupindukia sambamba na sera ya kuboresha viwango vya elimu , matibabu na miundo msingi kwa raia wake.

Sasa inasema ni asilimia moja tu ya Wachina walio na umaskini wa kupindukia.

Lakini kwa idadi ya watu zaidi ya billioni moja -bado hiyo ni idadi kubwa ya watu.

Katika kipindi cha miezi mitatu maafisa wamewadai wale wote waliochunguzwa na kupatikana kufuja fedha hizo badala ya kuanzisha miradi ya kujiendeleza - na hadi sasa dolla milioni

100 zimetaifishwa.

Mada zinazohusiana