Rais mteule George Weah awataka raia wa Liberia walio nchi za kigeni kurudi nyumbani kuijenga nchi

Weah awataka raia wa Liberia walio nje kurudi kuijenga nchi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Weah awataka raia wa Liberia walio nje kurudi kuijenga nchi

Rais aliyechaguliwa nchini Liberia George Weah, amewashauri raia wa Liberia wanaoishi nchi za ng'ambo kurudi nyumbani ili kusaidia kuijenga nchi yao.

Alitoa wito huo wakati wa mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu atangazwe mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Nyota huyo wa zamani wa kandanda alisema ujuzi wa watu wa Liberia walio nchi za kigeni unahitajika kuijenga nchi hiyo.

Bw. Weah alipongezwa aliposema kuwa ufisadi hautavumiliwa katika utawala wake. Anaingia madarakani rasmi mwezi Januari.