Maandamano ya kumtaka Rais Kabila aondoke madarakani yashuhudiwa Kinshasa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joseph Kabila

Askari wa usalama katika Jmahuri ya Demokrasi ya Congo, walitumia gesi ya jutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu, Kinshasa, ambao wanataka Rais Joseph Kabila, aondoke madarakani.

Mapambano yalitokea nje ya kanisa, ambapo waandamanaji walitaraji kujumuika katika mkutano ulioitishwa na makundi mbalimbali, pamoja na wanaharakati wa Kanisa Katoliki.

Wakuu mjini Kinshasa, walionya kuwa mkutano huo haukuruhusiwa.

Serikali imeamrisha kuwa mawasiliano katika mtandao wa internet yafungwe kwa muda.

Maandamano yaliitishwa kudai kuwa Rais Kabila afuate makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana, kwamba ataondoka madarakani kabla ya uchaguzi.