Sheria ya kuharamisha biashara ya pembe za ndovu yatekelezwa China

Pembe za ndovu zikiteketezwa moto nchini Kenya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pembe za ndovu zikiteketezwa moto nchini Kenya

Sheria iliyopiga marufuku kabisa biashara ya pembe za ndovu, imeanza kutekelezwa Uchina hii leo.

Vikwazo zilianza kufu-atwa katika miezi 12 iliyopita lakini sasa, hairuhusiwi kabisa kwa raia wa Uchina, kununua kitu chochote chenye pembe, ndani na nje ya nchi.

Taarifa ya serikali imesema, mfanyabiashara yeyote, anayejidai kwamba anauza pembe iliyopata kibali cha serikali, atakuwa anadanganya.

Uchina ilikuwa soko kubwa la meno ya tembo, soko ambalo limesababisha uwindaji kuzidi katika mbuga za Afrika.

Mada zinazohusiana