Wapalestina wamuita balozi wao kutoka Marekani

Jerusalem
Image caption Wapalestina wamuita balozi wao kutoka Marekani

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anasema kuwa hawezi kamwe kukubali mpango wowote wa amani wa Marekani kufuatia hatua hiyo ya Trump.

Maandamano yalizuka katika ukanda wa Gaza baada ya tangazo hilo.

Azimio la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta tangazo hilo lake liliunga mkono kwa wingi na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Wapalestina 13 wameuawa kwenye ghasia kufuatia tangazo hilo la Trump wengi wakiuawa wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel.

Mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na wapalestina.

Israel ilitwaa eneo la mashariki mwa mji, ambalo awali likuwa linakaliwa na Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya masahariki ya kati na inadai kuwa mji huo wote ni wake.

Leo Jumapili Bw Abbas aliutaja Jerusalem kuwa mji mkuu wa kiroho wa watu wa Palestina.

Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni hatua ambayo haijatambuliwa kimataifa, na nchi zote zimeweka balozi zao huko Tel Aviv.

Hata hiyo Rais Trump ameiambia wizara ya mashauri ya nchi kigeni kuanza mchakato wa kuhamisha ubalozi wa Marekani kwenda Jerusalem.

Wapalestina wametangaza kuwa wamemuita balozi wao kutoka nchini Marekani kwa mazungumzo, wiki kadhaa baada ya rais Donald Trump kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Mada zinazohusiana