Watalii 10 raia wa Marekani wafariki kwenye ajali ya ndege Costa Rica

plane wreckage Haki miliki ya picha Public Security Ministry
Image caption Watalii 10 raia wa Marekani wafariki kwenye ajali ya ndege Costa Rica

Watu 12 wameuwa kwenye ajali ya ndege magharibi mwa Costa Rica.

Kumi kati ya wale waliouwa walikuwa ni raia wa Marekani akiwemo rubani raia wa Costa Rica na rubani msaidizi.

Vyombo vya habari vilisema kuwa watano kati ya wale waliouawa walitoka familia moja.

Ripoti zinasema kuwa ndege hiyo ya injini moja ya Cessna 208 Caravan, ilikuwa safarini kutoka mji mkuu San José kwenda Punta Islita ambalo ni eneo la kistarehe.

Hukukuwa na manusura na wala haibainiki ni nini kilisababisha ajali hiyo.

Kisa hicho kilitokea katika eneo la milima karibu na Bejuco mkoa wa Guanacaste

Rais wa Costa Rica alithibitisha ajali hiyo katika taarifa iliyochapishwa mitandaoni akisema kuwa serikali yake imesikitishwa sana na vifo hivyo.

Mtangulizi wake rais wa zamani Laura Chinchilla, aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa mmoja wa wahudumuwa marubani alikuwa na binamu wake.

Image caption Watalii 10 raia wa Marekani wafariki kwenye ajali ya ndege Costa Rica

Mada zinazohusiana