Kim Jong-un: Kibonyezo cha silaha za nyuklia kiko kwenye meza yangu

People watch a television news broadcast showing North Korean leader Kim Jong-Un"s New Year"s speech, at a railway station in Seoul on January 1, 2018. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Jong-un: Kibonyezo cha silaha za nyuklia kiko kwenye meza yangu

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa na kibonyezo cha silaha za nyuklia kwenye meza yake wakati wote na hivyo Marekani isithubutu kuanza vita.

Katika hotuba ya mwaka mpya iliyopeperushwa kwa njia ya runinga, alisema kuwa Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskania akiongeza kuwa huo ni kweli na wala sio vitisho.

Lakini pia alitoa wito kwa Korea Kusini kuja kwenye mazungumzo.

Korea Kaskazini pia itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msikmu wa baridi nchini Korea Kusini, Kim alisema.

Wakati aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu vitisho vya Kim, Rais wa Marekani alisema, "tutaona, tutaona".

Alikuwa akizungumza kando mwa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika eneo lake ya kifahari la Mar-a-Lago huko Florida.

Korea Kaskazini imewekewa vikwazo zaidi mwaka uliopita kwa kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia na majaribio ya mara kwa mara ya silaha hizo.

Taifa hilo lililotemgwa lilifanya majaribio 6 ya nyuklia ya chini ya ardhi na kuonyesha kuongeza uwo wake wa makombora

Mwezi Novemba ilifanyia majaribio kombora lake la Hwasong-15 ambalo lilipaa umbali wa kilomita 4,475 mara kumi zaidi kuliko kituo cha safari za anga za juu.

Image caption Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini