Magari 1,400 yateketea kwenye mkasa wa moto Liverpool

Fire at the car park Haki miliki ya picha PA
Image caption Magari 1,400 yateketea kwenye mkasa wa moto Liverpool

Moto mkubwa umeharibu karibu magari 1,400 kwenye jengo la ghorofa la kuegesha magari huko Liverpool na kuwalazimu watu wengi kuukaribisha mwaka kwenye makao ya muda.

Wazima moto walisema kuwa moto huo katika jengo la King's Dock karibu na ukumbi wa Liverpool Echo Arena, ni mioto mibaya zaidi kuwai kukabiliana nayo

Haki miliki ya picha @NeuraPhoto
Image caption Magari 1,400 yateketea kwenye mkasa wa moto Liverpool

Polisi walisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa moto kutoka kwa gari ulisambaa kwenda kwa mengine.

Watu walihamishwa kutoka majengo yalito karibu kutokana na moshi.

Polisi wa Merseyside walisema kuwa magari ya kuzima moto 21 yalikuwa eneo hilo na huma za wazima moto zilesema zilikuwa zinachukua tahadhari ya jengo hilo kuporomoka.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Magari 1,400 yateketea kwenye mkasa wa moto Liverpool

Magari yote yaliyokuwa kwenye jengo hilo linaloweza kuegeshwa magari 1600 yaliharibiwa. kwa mujibu wa polisi.

Waliwashauri watu kubaki manyumbani mwao na kufunga madirisha ikiwa wangeona moshi kutoka kwa moto huo.

Mada zinazohusiana