Njia bora ya kutimiza malengo na maazimio ya Mwaka Mpya

feet in trainers running Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa kawaida, Mwaka Mpya unapowadia, watu hujiwekea maazimio na malengo mengi ya kutimiza katika mwaka huo.

Mara nyingi huwa ni kupunguza uzani, kufanya mazoezi zaidi, kuacha kuvuta sigara, kujifunza lugha mpya na kadhalika.

Lakini mara nyingi malengo haya huwa hayatimizwi.

Hatuwezi kukwambia ni maazimio gani unafaa kuyafanya, lakini kuna utafiti uliofanywa ambao unaweza kukuelekeza jinsi ya kujiwekea malengo ambayo utaweza kuyatimiza na pia njia bora zaidi ya kuhakikisha unatimiza malengo hayo.

Kuna ushahidi kwamba mara nyingi binadamu huongozwa na hamu ya "kupunguza hasara" - yaani, huwa mara nyingi tunaongozwa na kufuta hasara ambayo tumepata badala ya kupiga hatua mbele.

Kuweka maazimio kwa njia ambayo lengo lako zaidi litakuwa kupunguza au kufuta hasara, kwa maana ya kupata kitu ulichokipoteza, huenda yakawa rahisi kutimiza kuliko maazimio ya kukipata kitu kipya.

Mfano, inaweza kuwa rahisi kwako kuurejelea uraibu uliokuwa nao awali au kujiweka sawa kimwili kufikia kiwango cha awali kuliko kuboresha muonekano wako au uwezo wako kufikia viwango ambavyo haujawahi kuvifikia awali.

Hili pia linatuelekeza kwa ushauri mwingine muhimu unapojiwekea malengo yako ya mwaka - kabla lazima yawe ya uhalisia, yanaweza kutimizika.

Haki miliki ya picha Getty Images

Washirikishe wengine

Mwanafalsafa katika Chuo Kikuu cha Warwick Dkt John Michael hutafiti kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii yanayowasaidia watu kutimiza malengo na ahadi zao.

Anasema kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kutimiza ahadi na maazimio iwapo tutayatazama kwamba yana umuhimu kwa watu wengine - kwamba maslahi ya wengine yatakuwa hatarini iwapo tutashindwa.

Hii huenda ikawa ni kwenda darasani na rafiki yao.

Ufanisi unaweza kuwa hata zaidi iwapo utalipa karo mapema - ukihisi kwamba mtu amewekeza pesa na muda wake, na kwamba vyote vitapotea, basi kuna uwezekano kwamba utajizatiti kutimiza malengo hayo.

Utafiti wa Dkt Michael pia unaonesha kwamba watu huenda wakahamasishwa kuendelea na kazi wasiyoipenda iwapo mtu mwingine wa maana kwao amewekeza kitu hapo.

Vitu vya kukukumbusha

Sifa na hadhi ya mtu huwa muhimu sana, na vinaweza kutumika kama kichocheo.

Kuyafanya maazimio yako wazi kunaweza kukuhamasisha kuyatimiza kwani utahofia kwamba hadhi yako itashuka iwapo hutayatimiza.

"Huwa hakuna anayetaka kupata sifa za kuwa mtu asiyeaminika, kwa hivyo hutangaza mipango yetu hadharani kunaweza kutupatia motisha. Kuweka dau kunaweza pia kuwa kichocheo zaidi," anasema Prof Neil Levy wa Chuo Kikuu cha Oxford.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kuweka maelezo zaidi na ufafanuzi kwenye maazimio yako pia husaidia, anasema.

Mfano kwenda kwenye chumba cha mazoezi Jumanne alasiri na Jumamosi asubuhi, kwa mfano, ni bora kuliko kusema tu kwamba utaenda kufanya mazoezi mara nyingi zaidi, anasema Prof Levy.

Anapendekeza uhusishe maazimio yako na viashiria au vitu fulani vya kukukumbusha.

Iwapo unataka kujifunza lugha nyingine, unaweza kwanza kuweka ahadi ya kusikiliza makala ya lugha hiyo kila asubuhi ukisafiri kwenda kazini asubuhi.

Kisha, ndipo ujiwekee nafasi ya kufanikiwa zaidi, unaweza kuweka ujumbe wa kukukumbusha kufanya hivyo kwenye kidhibiti mweleko wa gari kila jioni kabla ya kulala.

Hapo, unaeleza nia na pia kuchukua hatua kuhakikisha unaitekeleza nia hiyo.

Kuweka masharti

Prof Levy anaonya pia dhidi ya kujiwekea masharti ambayo yanaweza kuwa vielelezo baadaye.

"Kubali wazi kwamba kuna baadhi ya mambo yanayoweza kukuzuia kufanya jambo (Sitakwenda kwa mazoezi iwapo nyumba itashika moto). Lakini usipanue masharti haya au kuyafanya kuwa mtindo kwani yanaweza kukuzuia kutekeleza maazimio yako.

"Siku yangu ya kuzaliwa, inaweza kuwa siku ya kipekee na inakubalika. Lakini nikianza kutambua mambo yanayofanyika mara kwa mara - pengine iwapo ni wiki ya mwisho ya mwezi, kuwepo kwa baridi kali - basi itakuwa mazoea," anasema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yafanye maazimio yako kuwa sehemu ya mipango yako ya muda mrefu

Kufanya maazimio kuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu

Kwa Dkt Anne Swinbourne, mwanasaikolojia katika chuo kikuu cha James Cook, Australia, maazimio bora zaidi ni yale ambayo yanaoana na malengo ya muda mrefu ambayo umejiwekea wewe binafsi, kuliko yale ambayo hayana msingi au ni matamanio tu.

Iwapo hujawahi kuonesha nia ya kushiriki katika michezo, kujiwekea malengo ya kuwa mwanariadha stadi ni lengo ambalo bila shaka utatatizika kutimiza.

Kwa sababu umekwua na ndoto ya muda mrefu ya kusafiri sana kujionea ulimwengu kabla ya kutimiza miaka 50, lengo la kusafiri zaidi linaweza kutimizika.

Na pia, kutimiza malengo yote hutegemea mipango yako.

Tambua ni mambo gani yanakuchochea kufanya mambo usiyoyapenda au usiyoyapenda. Iwapo hutaki kunywa pombe sana, panga kukutana na marafiki au wageni wako kwenye mgahawa badala ya baa, vilevile, ukipanda kuacha kuvuta sigara, vyema zaidi ni kuacha kujihusisha na wavutaji sigara sana.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii