Waandamanaji wajihami kwa silaha Iran

Maandamano yaendelea Iran,wana uslama washambuliwa na silaha Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maandamano yaendelea Iran,wana uslama washambuliwa na silaha

Polisi mmoja nchini Iran ameuawa kwa kupigwa risasi na waandamanaji wanaoipinga serikali ya taifa hilo maeneo mbali mbali nchini humo.

Msemaji wa Polisi amesema kuwa waandamanaji waliojihami kwa bunduki aina ya rifle wamekuwa wakifyatua risasi kati kati mwa mji wa Najafabad.

Hili ni tukio la kwanza kuuawa kwa afisa usalama tangu hali ya vurugu hizo ilipoanza siku ya alhamis.

Kumekuwa na taarifa za machafuko zaidi katika maeneo mbali mbali ikiwemo mji mkuu wa Tehran.

Hadi sasa watu 13 wameuawa kutokana na vurugu hizo,japo kuwa hapo awali rais Hassan Rouhani alikaririwa akisema kuwa waandamanji hao hawawezi kusababisha madhara yoyote.