Balozi wa Palestina nchini Marekani aamrishwa kurudi Washington

Jerusalem
Image caption Balozi wa Palestina huko Marekani ameamrishwa kurudi Washington

Mjumbe wa Palestina huko Marekani anasema anarudi Marekani baada ya mazungumzo wa siku moja kufuatia uamuzi wa Trump ya kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Husam Zomlot alisema alikutana kisiri na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Aliamrisha kurudi Marekani mara moja, alisema.

Siku ya Jumapili Bw. Abbas alisema kuwa hatakubali makubaliano yoyote ya amani ya Marekani kufuatia hatua hiyo ya Trump.

Mji wa Jurusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina na tangazo la Marekani la tarehe 6 Disemba lilisababisha maandamano kwenye ukanda wa Gaza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapalestina wanadai East Jerusalem ni mji mkuu wa taifa lao la baadaye

Azimio la Umoja wa Mataifa lililoitaka Marekani kufuta uamuzi huo liliungwa mkono pakubwa na baraza kuu la Umoja wa Maraifa

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Palestina Riad al-Maliki Jumapili kuwa mazungumzo kati ya Bw. Zomlot na Abbas uliandaliwa kufanya uamuzi unaohitajika na utawala wa palestina kuhusu uamuzi huo wa Marekani.

Wapalestina 13 wamefariki kwenyr ghasia tangu Trump atoe tangazo la kuutambua Jerusalem kufutia makabiliano na vikosi vya Israel.

Wapalestina wanadai East Jerusalem ni mji mkuu wa taifa lao la baadaye na hatma yake inatarajiwa kuzungumziwa wakati wa hatua za mwisho mwisho za mazungumzo ya amani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii