Korea Kusini yapendekeza mazungumzo ya juu na Kaskazini kuhusu Olimpiki

The logo for the 2018 Pyeongchang Winter Olympics is unveiled Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Ni wachezaji wawili pekee wa Korea Kaskazini walifuzu kwa michezo hiyo itakayoandaliwa Pyeongchang

Korea Kusini imetoa ombi la kutaka kufanyika mazungumo ya juu na Korea Kasuni tarehe 9 mwezi huu kujadili ikiwa kuna uwezekano wa kushiriki mashindano ya masimu wa baridi mwaka 2018.

Hii ni baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kusema kuwa alikuwa anatafikiria kutuma timu kwenda Pyeongchang nchini Korea Kusini kwa mashindano hayo mwezi Januari.

Alisema kuwa nchi hizo mbili zinahitaji kukutana kwa dharura kuzungmzia uwezekano wa kushiriki mashindano hayo.

Mapema rais wa Korea Kusini alisema kuwa ameiona hiyo kama fursa ya kuboresha uhusiano ulioharibika kati ya nchi hizo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Jong-un alisema kuwa alikuwa anafikiria kutuma timu kwenda Pyeongchang nchini Korea Kusini kwa mashindano hayo mwezi Januari.

Waziri wa mapatano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon alipendekeza Jumanne kuwa wawakilishi watakutana katika kijiji ya mapatano cha Panmunjon.

Kijiji hicho kilicho eneo lenye ulinzi mkali la DMZ mpakani ndipo mazungumzo kati ya nchi hizo yamekuwa yakifanyika.

Bado haujulikani ni nani atahudhuria mazungumzo hayo ya tarehe tisa Januari, na Korea Kaskazinia bado haijajibu.

Mazungumzo ya mwsiho ya juu yalifanyika Disemba mwaka 2015 katika eneo la pamoja la viwanda la Kaesong.

Yalimalizika bila makubaliano yoyote na ajenga ya mazungumzo haikutangazwa.

Mada zinazohusiana